Huu ni wivu au!!??

Zacharia Kifyasi

Senior Member
Joined
Dec 23, 2012
Posts
135
Reaction score
24
Nina mpenzi wangu (mjita) ambae nimedumu nae kwa zaidi ya miaka miwili na nusu sasa, tunapendana sana kwenye shida raha kwani ameridhika na hali yangu ya kimaisha! Alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni moja hivi hapa dar, lakini miezi miwili hivi iliyopita aliamua kuacha kazi kwa madai kuwa haina maslahi hivyo akaniambia anaenda kwa wazazi wake Morogoro, anaenda kutulia nyumbani.
Hapa ninapo kaa niko karibu na dada yake ambae amepanga jirani na nyumba ninayo kaa,. Huyu dada yake ana house girl. Tatizo ni kwamba huyu house girl akipita nyumbani nikapiga nae story mbili tatu huyu dada mtu ana mpigia mdogowake simu kuwa naongea na house girl wake, baada ya hapo mpenzi wangu anacharuka na kutishia kwamba tuachane. Hapa nimechoka nikiangalia hapa nyumbani ndio njia ya huyu house girl kupita, sasa nisioongee nae jamani kisa ntamtongoza? Wadau huyu dada mtu mwenyewe ana mimba kubwa yani nashindwa hata kumfuata kumweleza upuuzi wake!
 
Tatizo nyie wanaume huwa hamcheleweshi.. Nikwanini ung'ang'anie kuongea na huyo house g morever ushajua kwamba yendo source.. Maana nyie mtu akikuzoea tu basi unaona easy to get
 
sasa na wewe kwan lazima huongee na huyo house g!
 
Tatizo nyie wanaume huwa hamcheleweshi.. Nikwanini ung'ang'anie kuongea na huyo house g morever ushajua kwamba yendo source.. Maana nyie mtu akikuzoea tu basi unaona easy to get

Sio kwamba nimemng'ang'ania, yani ni sawa na wewe unakutana na jirani yako alafu mnasalimiana na kuongea maneno mawili au zaidi hiyo ndio shida jaman?
 
kama mnapendana muoane muishi pamoja hayo matatizo yataisha wakat meingine uyo mpenz wako anapewa sumu kali na uyo dada.

hiyo sumu inaongezwa na chumvi. kama vip muishi wote siku hazigandi.
 
Sio kwamba nimemng'ang'ania, yani ni sawa na wewe unakutana na jirani yako alafu mnasalimiana na kuongea maneno mawili au zaidi hiyo ndio shida jaman?

maneno mawili yanini ili iweje.. Salam fupi tu yatosha acha mazoea ya kijinga after law huyo house g wao ndo wanamjua kuliko wewe after law siyo ndugu yake
 
Mwambie arudi zake haraka, kama ameshawaona wazee inatosha. sasa anataka wewe upikiwe na nani, uzungumze na nani, huwezi kukaa kimya tu kama bubu..
 
Kwanin ukazane kuongea naye wakt mwenzako hatak??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…