Huu ni utapeli mpya?

Ni aina mpya ya utapeli. Nilipigiwa simu na mtu aliyedai ni mwalimu wa shule ya mwanangu akajitambulisha anaitwa Mwl. Fredrick,na kweli shule hiyo ina mwalimu mwenye hilo jina,akasema mwanangu amepata ajali amegongwa na pikipiki wamemkimbiza hospitali na anatakiwa kuongezewa damu haraka sana hivyo nitume elfu 50, nilipata mshtuko uliochanganyika na bumbuwazi,nikawaza kukimbia hosp lakini ni 30km kutoka hapa,nikapata wazo nitume kwanza hiyo pesa mtoto awekewe damu nisimpoteze mwanangu. Kabla sijatuma akili ikanijia, msaidizi wa mwalimu mkuu ni rafiki yangu,kwa nini hakunipa taarifa mpaka wampeleke hosp mbali hivyo wakati kuna hospitali kubwa private hapa jirani...nikasema ngoja nimpigie,nimemsalimia akaitikia kwa bashasha kuonesha yuko okay hakuna jambo la hatari,nikajiambia labda hata taarifa za ajali ya mwanangu,nikampa pole nikamuuliza imekuwaje wampeleke mtoto hospitali mbali badala ya kumpatia huduma za haraka hapa jirani akashangaa akaniuliza mtoto gani, nikamwambia taarifa niliyopewa kuhusu ajali ya mtoto, akacheka sana..daaah...akaniambia umeshaliwa,nikamwambia sijatuma ndio niko kwenye mchakato akaniambia wewe ni mazazi wa pili unapewa taarifa kama hii ila mwenzako ametapeliwa na pesa akatuma .

Nilichoka sana, baadae wananipigia wananiambia niharakishe nikawaambia simameni hapo hapo subirini pesa, wakanitukana mngese sana wewe wakakata simu.

Jamaa wanashtua sana hawa.
 
Mimi leo nimetumiwa sms eti nimeshinda m60 ya tatu mzuka na ata sijawahi kucheza na sijui wanachezaje eti wakaweka na namba niwapigie huu nao ni uhuni pia.
 
Duuuu pole sana.
 
Siku hizi matapeli wamekuwa wengi sana, wengine hata akili hawana lakini nao eti ni matapeli badala ya kuwa vibaka tu.
 
Hilo lilikuwa jaribio sio utapeli, wangefanikiwa ungeita utapeli, ila mpaka hatua hiyo ni jaribio lililo fail!
 
Watu kama nyie ndio mnaikuza hii tasnia ya utapeli.

Yaani hata bila kuuliza tarifa za kutosha na ukataka kutuma pesa?
 


Siku nyingine walengeshe kwa polisi au kodi mabaunsa 6 wa kuwanasa, dunia ya sasa ni ya kuishi kwa akili x 10
 
Pole mamy wangekuliza
Mm huwa napigiwa simu na hawa matapeli wanajifanya customer care wa tigo anaanza eti kukuuliza unaitwa nani nawajibu tu acheni utapeli wenu wanakata simu mara nyingi tu huwa wananipigia
 
Bahati mbaya baadhi ya hao matapeli wameshasoma huu uzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…