Huu ni ujumbe kwa JK

Huu ni ujumbe kwa JK

nakuru

Member
Joined
Apr 5, 2012
Posts
88
Reaction score
22
Awali ya yote nakupa pole kwa majukumu makubwa ya kuliongoza taifa hili, kwa katiba tulikuwa nayo natambua kuwa una majukumu, maamuzi makubwa sana tena mazito kwa taifa hili kwani kila kitu ni wewe n a kwakuwa wewe ni binaadamu wa kawaida kama mimi kwa mamlaka uliyopewa na katiba unaweza kufanya na umefanya mambo ambayo ni sahihi na mengine si sahihi kwa taifa, aidha kwa utashi wako au kwa kuwasikiliza washauri wako, yale ambayo si sahihi hakuna kipingamiza kwamba yatakugharimun wewe kama kiongozi ambaye umepewa dhamanana ya kuongoza taifa hili.

Sasa hivi kila pembe ya Tanzania kuna fukuto la ya kudai haki sawa, rasimali za taifa kusaidia watanzania wote na si wachache kama ilivyo………….nikimaanisha viongozi wa serikali yako na wawekezaji (wageni) natumai hili unalitambua na kama hulitambui basi unayo hasara na bahati mbaya!

Mimi ni kijana (sis indo taifa la kesho) wa Tanzania lakini napenda kukuambia kwamba Tanzania ya sasa si ile ya baba wa taifa, si ile ya raisi mwinyi (mzee ruksa) na si ile ya mzee mkapa (zama za uwazi na ukweli…..slogan hii ilikuwa kinyume kwani zilikuwa zama za uficho na uongo) awamu hii ni awamu ya dunia imekuwa kijiji, ni awamu ya "digital" (dot com) sisi vijana tumegundua jinsi Mungu alivyoibariki hii nchi , jinsi rasilimali za nchi hii zinawanufaisha wageni na viongozi wa serikali ya ccm (tunaamini huu si mpango wa Mungu kuibariki hii nchi kwa ajili ya wachache), na nina amini hili unalitambua.

Ninajua wewe ni mwenyekiti wa ccm taifa na umebakiza miaka 2 uachie madaraka ya uraisi, sasa ninachokiona kwenye uongozi wako katika hizi dakika za lala salama unaangalia ccm kwanza badala ya kuangalia Tanzania kwanza; Kaka yangu ukiendelea kuangalia ccm kwanza badala ya taifa utakuja kujilaumu pamoja na hawo wanokushauri na ninadhubutu kusema kwamba pamoja na dola ambayo unayo inawezekana kabisa hii miaka yako ya uraisi iliyobaki yaani kufikia 2015 isifike kutokana na fukuto lililoenea nchi nzima.

Na nasema hili kwani serikali yako inatumia kila mbinu ili ipate ridhaa kwa wananchi na mbaya zaidi seriklai yako imefanikiwa pia kulikteka bunge ili kufunika mauvo na ufisadi wa serikali yako……….hili la kuteka bunge mnaweza kufikiri/kuona ni hatua nzuri kimafanikio kwa ccm lakini nasema ni hatua hatari sana na mbaya sana kwa taifa……kumbuka kuwa mfugaji anaweza kutumia mbinu zote kumpeleka ngombe mtoni hata kama hataki kwenda lakini hamwezi kutumia mbinu zote ili anywe maji!

Ushauri;

kwa mamlaka ambayo umepewa na katiba; tumie zaidi utashi wako kuliko washauri ili uwache taifa mahali salama nawe pia uwe salama, kwani watanzania hasa vijana wamekinai na kuchoka na uongozi wa serikali ya ccm (acha demokrasia ichukue mkondo wake kwani maji hayapandi kilimani) Vita na machafuko ni vitu vibaya sana na kumbuka vita haina macho, ushauri huu ninakupa si kwasababu nina kupenda sana wala kwa sababu mimi ni mwana CCM bali ninauotoa kwasababu mimi ni Mtanzania na ninaipenda san nchi yangu, kumbuka machafuko na vita yanaweza kutokea mahali popote na dakika yoyote na yanaweza kuletwa na kitu/sababu ndogo sana mfano mzuri ni nchi ya TUNISA.

Raisi wangu soma alama za nyakati na tambua kuwa Watanzania ni binaadamu na wana roho sawa na Wa-tunis, wa-kenya na wa-misri na wa-libya! Taifa kwanza, ccm baadaye! Mungu saidia Tanzania ipate uhuru. AMEN.
 
Edit na weka paragraph.... vizuri usomeke, kwani unaumiza macho kweliiiiiii......
 
...niliwahi kusikia eti ni msikvu, ila sijawaahi kusikia kuwa ni mwelevu.... akipata mtu wa kumsomea atakusikia.
 
Nadhani ataupata ujumbe huu muhimu sana. TAIFA KWANZA, CCM BAADAE.
 
kama hujasoma na kuelewa unatakiwa urudi darasani, ingekuwa english ungesemaje?
 
Unalalamika mno, kijana wa sasa halalamiki anafanya kazi ili kujipatia kipato cha kukidhi mahitaji ya maisha yake
 
Unalalamika mno, kijana wa sasa halalamiki anafanya kazi ili kujipatia kipato cha kukidhi mahitaji ya maisha yake

Mkuu ni vyema ukasoma post ya mleta mada kisha ndo ukaanza kuchangia, na siyo kukurupuka kama nyumbu.
 
Back
Top Bottom