Habari wana JF,
Rejea Kichwa cha habari tajwa hapo juu.
TBS wameonesha ubaguzi mkubwa Sana katika hilo tangazo Kwa kigezo cha transcripts zisiwe zimezidi mwaka mmoja tangu mwanafunzi alipo hitimu masomo yake.
Hii inakinzana kabisa na ofisi za umma kutoa nafasi Sawa kwa watanzania wote wenye sifa pasi kuangalia walihitimu lini masomo yao.
Angalia kipengele namba III, kijistari (-) cha pili.
Hasa Ukizingatia kuwa kigezo cha umri tu kimeisha waondoa wengi wenye zaidi ya 35.
Ikumbukwe, kuwa hizi kada za science mara nyingi ajira zake ni chache sana.
Kwa hiyo waliohitimu zaidi ya miaka 3-5 bado wapo wengi mitaani wakitafuta ajira. Ambao techincally, wanaweza wakawa kwenye umri wa 26-30. Ila, kwa ubaguzi huo wa kuhitimu masomo si zaidi ya mwaka unakuwa umewanyima haki kundi kubwa hapa.
Ikumbukwe sipo Tanzania wala sina mtu anayehitaji kazi hapo Tanzania Bureau of Standards (TBS).
Natambua kuwa kila mtu atakuwa na mawazo mbadala yote yanapokelewa maana ndiyo maana ya mjadala huu.
Niwatakieni ,mchanganuo mzuri juu ya hili tangazo
Weekend njema.
Chanzo:- TBS website.
— Tanzania Bureau of Standards (TBS)
Utawapa mitaji?SULUHISHO LA HAYA YOTE NI KUJIAJIRI.
Kwani ni lazima ukiwa na Degree au Masters au PhD uajiriwe? Nadhani sasa ni wakati muafaka kwa Elimu zetu tulizonazo zitusaidie katika kujiajiri kuliko kutegemea kuajiriwa kitu ambacho kwa aina ya Soko la Ajira lilivyo gumu na lenye ushndani kwa sasa ni usumbufu / kero kubwa.
Poise Nadhani suala la transcript kutozidi mwaka mmoja wapo sahihi. Mara baada ya kuhitimu unaweza kupewa transcript ambayo hutumika kwa muda tu kisha baada ya hapo unategemewa kuwa umepata cheti.Habari wana JF,
Rejea Kichwa cha habari tajwa hapo juu.
TBS wameonesha ubaguzi mkubwa Sana katika hilo tangazo Kwa kigezo cha transcripts zisiwe zimezidi mwaka mmoja tangu mwanafunzi alipo hitimu masomo yake.
Hii inakinzana kabisa na ofisi za umma kutoa nafasi Sawa kwa watanzania wote wenye sifa pasi kuangalia walihitimu lini masomo yao.
Angalia kipengele namba III, kijistari (-) cha pili.
Hasa Ukizingatia kuwa kigezo cha umri tu kimeisha waondoa wengi wenye zaidi ya 35.
Ikumbukwe, kuwa hizi kada za science mara nyingi ajira zake ni chache sana.
Kwa hiyo waliohitimu zaidi ya miaka 3-5 bado wapo wengi mitaani wakitafuta ajira. Ambao techincally, wanaweza wakawa kwenye umri wa 26-30. Ila, kwa ubaguzi huo wa kuhitimu masomo si zaidi ya mwaka unakuwa umewanyima haki kundi kubwa hapa.
Ikumbukwe sipo Tanzania wala sina mtu anayehitaji kazi hapo Tanzania Bureau of Standards (TBS).
Natambua kuwa kila mtu atakuwa na mawazo mbadala yote yanapokelewa maana ndiyo maana ya mjadala huu.
Niwatakieni ,mchanganuo mzuri juu ya hili tangazo
Weekend njema.
Chanzo:- TBS website.
— Tanzania Bureau of Standards (TBS)
Poise Nadhani suala la transcript kutozidi mwaka mmoja wapo sahihi. Mara baada ya kuhitimu unaweza kupewa transcript ambayo hutumika kwa muda tu kisha baada ya hapo unategemewa kuwa umepata cheti.
Hakuna chuo au shule ambayo transcript na cheti vinaweza kuchelewa zaidi ya mwaka labda kama kuna tatizo ambapo kwa vyovyote vile unaweza kuwa na ushahidi wa hilo.
Kutokuwa na cheti husika na kubaki ukitumia transcript kwa muda mrefu ni ishara ya kuwa uenda kuna vitu hukukamilisha pale ulipokuwa unasomea. Vipo vyuo vingine hutoa transcript nusu nusu kwa kadili unavyomaliza courses zako na hivyo ni rahisi mtu kutumia hizo hata kama hajamaliza. Si kila mwajiri atatambua kwa haraka course ulizotakiwa kusoma na wengine miaka inatofautiana. Kuonesha kuwa ulihitimu basi weka cheti na kama cheti hakijatoka weka transcript ambayo haiwezi kuwa zaidi ya mwaka toka umemaliza maana kwa vyovyote vile cheti kinakuwa tayari kimetoka. Kama kuna sababu za kuchelewa kiambie chuo kikupatie barua maana hufanya hivyo.
Suala la umri nalo ni debatable, pengine TBS hutumia resources zao kutrain wafanyakazi wao ili wafanye kazi kwa kiwango stahiki. Sasa katika kutimiza hilo ni lazima uwe na watu ambao angalau unao uhakika wa kuwa nao kwa muda mrefu zaidi. Unamchukua mtu wa miaka 45-50 unaanza kumpika mpaka anakuwa mbobezi labda miaka 5. Kisha anafanya kazi miaka 5-10 anastaafu sasa hiyo si hasara.
Pili wengi wa watu wa miaka 35+ tayari wana kazi na uzoefu hivyo si busara pia kuwapambanisha na graduate ambao pengine hawana uzoefu, na ndo vijana unaowatarget ili uwapike kwa kulingana na kazi yako. Acha vijana wapate fursa ya kutumikia nchi yao kwa muda mrefu wale wanaotaka kubadili kazi waangalie fursa zingine.
Kigezo cha umri utumika mahali pengi, ikiwemo jeshini, TISS. Bahati nzuri umesema huko nje, basi hata huko usijifungie ofisini, au chuoni au mahali unapobeba box tu. Huko huwa na vigezo hata kwa mwanafunzi wanayemdahili kwa ajili ya PhD au Masters na hasa kama wanakupa scholarship. Wanaangalia unaweza kusaidia jamii yako kwa muda gani sio wanainvest tu kupoteza hela.