Huu ni muda muafaka kwa nafasi ya Rais kusimamia anachokiamini.

NJUGHU

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
380
500
Watanzania tuungane katika hivi vita vya kiuchumi kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Kumekuwa na maneno mengi kwamba ni CCM ndio imetufikisha hapa, hakuna anaebisha maana hata wapinzani walikuwa wanaccm,kumbe tumefikishana hapa wote.

Vita hivi ni vigumu, Rais ameonyesha nia dhabiti,wapo wanadai mbona alikuwa kwenye serikali hii muda mrefu, hivi tujiulize;

-Kama yeye kondoo ndani ya mbwa mwitu angefanya nini kipindi hana mamlaka,si mbwa mwitu wangemgawana?

-Asingingevuta subira hata hiyo nafasi angeisikia kwenye radio,ukila na kipofu usimguse mkono wahenga walisema.

- Hata Mungu aliliokoa taifa la Israel kwa kumtupa Yusufu kwa wamisiri na kuwa mtawala huko,hivyo Magu ililidi apite CCM

Katika vita hivi tumuunge Rais bila kujali tutakosa au kupata lakini tusiendelee kuwa watumwa wa utajiri wetu.

Wapinzani kuna namna ya kuwakilisha mawazo yetu hata kuomba kuonana na Rais si kupitia media. Kuna wanasiasa watapoteza umaarufu wao kupitia sakata hili.

Tunaulizana viongozi wa awamu iliyopita hawajatajwa,sangara hutegwa kwa samaki mdogo kwenye ndoana!

Mahakama ya mafisadi itajaa tu.
Hii ni vita ya kizalendo.

Rais wetu kipenzi Makufuli Aluta continue.
 

mchoti tz

Member
Apr 14, 2017
31
95
Rasi wetu anajitaidi kadili ya uwezo wake ebu tumpe ushirikiano wa kutosha ili tuweze kufika hatua nzuri kimaendeleo
 

vampire_hunter007

JF-Expert Member
Jul 25, 2015
1,035
2,000
Hivi mnaposema tumpe ushirikiano huwa mnamaanisha nini? Ushirikiano upi? Asipoungwa mkono na baadhi ya watu anapungukiwa nini? Kipi ambacho kitakwama ikiwa baadhi ya watu hawamuungi mkono? Yani wabongo wanapenda sana kuongea bila kushirikisha ubongo
 

Kikarara78

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
1,493
2,000
Boss NJUGHU Ni kweli tumuunge Rais Mkono katika vita hii ya Uchumi. Chain yote wahojiwe kuanzia Top mpaka Dagaa, sio Dagaa tu. Pia mikataba yote ya Madini, Gas, Mafuta na Manunuzi iwekwe wazi pamoja na kupelekwa Bungeni.


Watanzania tuungane katika hivi vita vya kiuchumi kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Kumekuwa na maneno mengi kwamba ni CCM ndio imetufikisha hapa,hakuna anaebisha maana hata wapinzani walikuwa wanaccm,kumbe tumefikishana hapa wote.
Vita hivi ni vigumu,Rais ameonyesha nia dhabiti,wapo wanadai mbona alikuwa kwenye serikali hii muda mrefu,hivi tujiulize;
- kama yeye kondoo ndani ya mbwa mwitu angefanya nini kipindi hana mamlaka,si mbwa mwitu wangemgawana?
-asingingevuta subira hata hiyo nafasi angeisikia kwenye radio,ukila na kipofu usimguse mkono wahenga walisema.
- hata Mungu aliliokoa taifa la Israel kwa kumtupa Yusufu kwa wamisiri na kuwa mtawala huko,hivyo Magu ililidi apite CCM

Katika vita hivi tumuunge Rais bila kujali tutakosa au kupata lakini tusiendelee kuwa watumwa wa utajiri wetu.
Wapinzani kuna namna ya kuwakilisha mawazo yetu hata kuomba kuonana na Rais si kupitia media. Kuna wanasiasa watapoteza umaarufu wao kupitia sakata hili.
Tunaulizana viongozi wa awamu iliyopita hawajatajwa,sangara hutegwa kwa samaki mdogo kwenye ndoana!
Mahakama ya mafisadi itajaa tu.
Hii ni vita ya kizalendo.

Rais wetu kipenzi Makufuli Aluta continue.
 

habari ya hapa

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
12,809
2,000
Nitaanza kumuunga mkno na kumwombea daile pale atakapo weka wazi mkataba wa ununuzi wa ndege, ujenzi wa reli, na ujenzi wa uwanja ndege chato,
 

miwani ya maisha

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
1,608
2,000
Usanii tu tena msitake kuendelea kuchezea akili ZETU
Rais apitie kwanza mikataba ya kuuza nyumba za serkali aachane na maigizo ya kutukumbushia mambo aliyoyapigia MAKOFI KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI.

RAIS INABIDI ATUOMBE RADHI WATANZANIA KWA KUTUFANYA SISI RAIA KUWA MAZUZU!!

RAIS ANATAFUTA SIFA BINAFSI KWA KUTUDANGANYA MAMBO YASIO NA TIJA KWA MAISHA YETU..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom