Awiii Uwiii Awoo! ni vilio kila kona.
Viiana, wazee nao, alo salama hakuna,
Nchi ni maombolezo, mazikoni twapishana.
Tumwendee Mungu Baba, yeye ni mwenye rehema.
Awali tunakumbuka, virusi vilisheheni,
Pamoja tulianguka, tukaenda magotini,
Pasipo kuwa na shaka, pembezoni na mijini,
Mungu aliturehemu, dunia kuishangaza.
Imetupasa kujua, Mungu ndiye mwenye haki,
Huponya tukimwendea, ila uovu hataki,
Ataondoa balaa, na salama tutabaki,
Tukimrudia Baba, taifa litaokoka.
Sisi sote tumekosa, tumefanya machukizo.
Uovu tumetakasa, hila tumefanya nguzo.
Kila kukicha ni visa, uharifu ni gumzo,
Kwa macho yetu twaona, mwisho wa wetu uovu.
Wanaume wanawake, kabila na rangi zote,
Mungu na tumkumbuke, hata tukiwa fungate,
Akunje upanga wake, la sivyo twaisha sote.
Tukimwomba na kutubu, Mungu ataturehemu.