Hello wana JF,
Kuna siku bhana nimejaribu kuingia hii kupatana Dot Com. Mimi nina mtindo kama nataka kununua kitu Online huwa natest kwanza uaminifu wa wahusika. Nilikuwa nasoma tu thread za humu kwamba kumejaa matapeli kule sasa nami nikajitosa nijue huo utapeli.
Sasa bhnaa nikaona TV jamaa anauza yupo mkoa ambao naweza kupata hiyo bidhaa mapema na kuiona. Flat Screen bei aliyoweka ni laki 2 tu.Nikasema ngoja nijaribu kwa huyu ameweka namba zake ngoja nimtext kama akiwa na sound za kitapeli tu na hana ofisi ya kueleweka namtosa.
Meseji zetu zikawa
Me...flat screen zako ni mpya ? Na hiyo ya laki mbili ni aina gani? Na inch ngapi?
Jamaa...ndio laki mbili ni nchi 28 ambayo unatumiwa ulipo. Nazime baki 3 saivi wameshalipia.
Me...Ni Aina gani mkuu?
Jamaa....Nchi 28 na star x
Jamaa...Juma 3 naingia na mzigo tunaagiza Kongo ukiitaji weka oda kisha tusubiri juma3, napokelega Kigoma mizigo kutoka Kongo. Ukiitaji hiyo itakuja na Kirimanjaro bot mpaka Dar kisha Dar utaufata stend.
Jamaa....Saivi Imelipiwa moja tena zimebaki 2
Me...... Nielekeze ili nishuke baadae ofisin kwako
Jamaa.....Utakapo Kuwa tayali nijulishe .Utamkuta Mtu ofcn mimi sipo niwekuja kufata mizigo ya watu wa oda. Nasizani kama utaikuta hiyo unayo taka zilikua 20 toka asubuhi saivi imebaki moja, wakati mwema ukiwa tayal sema watakufata stend uliopo wakupeleke
Me....Ungenielekeza Ilipo ofisi ningekuja kuangalia nikiridhika na mzgo natoa pesa nakupa narudi na mzigo..
Sikujibiwa tena message...
Sasa siwezi sema jamaa ni tapeli ila kwa sound hizo kwangu ni kama tapeli.... Kwahiyo kuweni makini sana inawezekana kuna watu washaliwa pesa.Maana ukiulizia maduka ya tv hapa nilipo biashara ya tv si ya haraka kutoka kama jamaa anavyosema hapa juu mara zimebaki mbili sijui ngapi utadhani watu wananunua peremende.
hiv hatma yake ilikuwajehahahahahahaha
kuna dada alilizwa gari shoppers, likaondoka kama movie vile
lazima atakuwa ni mmoja wao si burewe ni wakala wao nini?
lazima atakuwa ni mmoja wao si bure
A typical Tanzanian answer! Majibu kama haya uliyotoa ndio imekuwa kama culture ya mtanzania. Mtanzania yoyote ukim-challenge au kumwonyesha udhaifu kwenye huduma anayotoa badala ya kukupa jibu la kuridhisha 1: Kwanza atafoka 2: Atakutolea mfano, na mara nyingi kutoka nchi zilizoendelea kuhalalisha udhaifu wake! Haya ni makosa makubwa! Inaelekea huenda wewe ni mmoja wa wamiliki wa huo mtaandao. Si mara ya kwanza bali ni mara nyingi nimeshakutana na malalamiko ta matapeli kugeuza site yenu kama kijiwe chao. Wewe badala ya kujaribu kuja suluhisho unataka kuhalalisha utapeli unaofanyika kwa kutumia sites nyingine kama role modelS wako! Siku watu wateja watakapoacha kutumia huduma yenu au akija mshindani mwenye mikakati zaidi utakimbilia kwa mganga ati umelogwa... na possibly mganga atakakuambia katafute mifupa ya albino..Kuwa na heshima na adabu, Hivi unajua namna ambavyo mtandao wa kupatana wanafanya kazi au unakurupuka tuu kucomment vitu ambavyo huna ufahamu navyo.?
kwa taarifa yako siyo kupatana tuu, mimi ni mteja mzuri sana wa online markets kuanzia ebay mpaka alibaba. kiufupi katika mitandao ya manunuzi kutapeliwa utake mwenyewe. Hata hao kupatana kama jinsi mtoa mada alivyotoa, ushaona muuzaji anabehave hivyo utakuwa ni ufala na uzoba ikiwa utatapeliwa kinamna hiyo.
Hiyo alibaba yenyewe watu wanalalamika kutapeliwa kila uchwao, lakini haiondoi uhalisia kuwa wapo watu wengi tuu wanaofanikiwa kununua bidhaa huko. mimi nikiwa mmoja wapo na ndiyo iliyomuingiza Jack Ma katika ulimwengu wa mabilionea wa dunia.
la muhimu watoe elimu kwa wateja wao ili waelewe matapeli wanaoharibu biasharaKuwa na heshima na adabu, Hivi unajua namna ambavyo mtandao wa kupatana wanafanya kazi au unakurupuka tuu kucomment vitu ambavyo huna ufahamu navyo.?
kwa taarifa yako siyo kupatana tuu, mimi ni mteja mzuri sana wa online markets kuanzia ebay mpaka alibaba. kiufupi katika mitandao ya manunuzi kutapeliwa utake mwenyewe. Hata hao kupatana kama jinsi mtoa mada alivyotoa, ushaona muuzaji anabehave hivyo utakuwa ni ufala na uzoba ikiwa utatapeliwa kinamna hiyo.
Hiyo alibaba yenyewe watu wanalalamika kutapeliwa kila uchwao, lakini haiondoi uhalisia kuwa wapo watu wengi tuu wanaofanikiwa kununua bidhaa huko. mimi nikiwa mmoja wapo na ndiyo iliyomuingiza Jack Ma katika ulimwengu wa mabilionea wa dunia.
A typical Tanzanian answer! Majibu kama haya uliyotoa ndio imekuwa kama culture ya mtanzania. Mtanzania yoyote ukim-challenge au kumwonyesha udhaifu kwenye huduma anayotoa badala ya kukupa jibu la kuridhisha 1: Kwanza atafoka 2: Atakutolea mfano, na mara nyingi kutoka nchi zilizoendelea kuhalalisha udhaifu wake! Haya ni makosa makubwa! Inaelekea huenda wewe ni mmoja wa wamiliki wa huo mtaandao. Si mara ya kwanza bali ni mara nyingi nimeshakutana na malalamiko ta matapeli kugeuza site yenu kama kijiwe chao. Wewe badala ya kujaribu kuja suluhisho unataka kuhalalisha utapeli unaofanyika kwa kutumia sites nyingine kama role modelS wako! Siku watu wateja watakapoacha kutumia huduma yenu au akija mshindani mwenye mikakati zaidi utakimbilia kwa mganga ati umelogwa... na possibly mganga atakakuambia katafute mifupa ya albino..
ushauri wangu: Jaribu kukubali wateja wanapokuonyesha loopholes zilizopo kwenye site yenu na muwe wabunifu katika kuzishughulikia. Na mwisho chungeni sana kauli zenu. Ukionyeshwa kosa 1. kubali 2. toa maelezo ya kiungwana kwanini udhaifu upo 3. Toa ushauri wa kiungwana jinsi wateja wanavyoweza kuepuka na ule udhaifu 4: Sema utajitahidi kadiri ya uwezo wako kulishughulikia 5. Rudi kwenye drawing table weka mikakati ya kulitanzua
Ndo maana Nimeandika Nilikuwa najaribu uaminifu wa Muhusika na Yeye mwenywe amesema Hapo kwamba Atanipeleka Ofisini.... It means anayoTatizo mleta mada umekariri sio watu wote wanaouza vitu mtandaoni hua wana maduka physically..mwingine anaweza kua anauza kitu lakini hana duka na hao kupatana wamekuandikia kwamba never pay in advance
Sijui kama na wewe unaelewa nilichoandika. Naona mnanibatiza vyeo visivyo vyangu mara sijui mimi ndo mmojawapo wa wezi, mara mimi ni mmiliki wa mtandao. Mimi si mmiliki wa mtandao wala siyo muuzaji wa vitu huko, bali ni mnunuzi wa vitu pekee. Sijui mnunuzi anamiliki vipi duka ama anamuibia vipi muuzaji.
Nikwambie tuu uzembe wako siyo excuse ya kujustify ili upate haki yako. Maana muongozo wa kupatana upo wazi kabisa na wameuandika katika website kuwa never pay in advance, sasa wewe unavyopay in advance huo ni uzembe wakona huna wa kumlaumu ukiibiwa.
Unasema sijui nimesafiri sijui najiona wa ulaya. Nikwambie tuu kuwa sijawahi kutoka nje ya tanzania hayo yote ya kununua viti ebay, alibaba nayafanya nikiwa tanzania na sijawahi ibiwa na mtu siri ni kuwa nilichukua muda wangu nikafanya homework juu ya manunuzi ya mitandaoni plus normal logics za kuzaliwa nazo and look, here nafurahia mtunda ya kazi.
Na nikwambie tuu sijasema kuwa hakuna wezi katika kupatana, wezi wapo na watu wema wapo. Kazi kwenu mnaokurupuka kufanya vitu msivyokuwa na uelewa navyo kwa sababu ya fasheni na ulimbukeni
Mimi nimeelewa ulichoandika kwani hukuandika kitu kigumu kueleweka bali umemfokea mwanzisha thread eti ''awe na heshima na adabu'' baada ya kuanzisha thread ya kuonya jinsi kulivyo na utapeli kwenye hiyo site! Hapa umeonyesha tatizo kubwa. Msitu una mbwa mwitu ametokea msamaria anawaonya wanaokatiza msitu ule wawe waangalifu wewe badala ya kushukuru unafoka? Umekuwa mbwa mwitu? Ni kweli kwenye internet kuna utapeli wa kina aina na anapotokea mtu akatahadharisha ni vizuri kwani kuna wageni wengi ambao hawajui. Wewe kama unajua na umeshafanya manunuzi sijui ebay nk usikataze wengine kujulishwa! Halafu mwanzisha thread hakusema wamiliki wa mtandao ndio wezi bali ameelezea kuwa kuna wauzaji wanaweza kuwa matapeli. Wewe ni nani mpaka ufoke? Ebo!Sijui kama na wewe unaelewa nilichoandika.
Mimi nimeelewa ulichoandika kwani hukuandika kitu kigumu kueleweka bali umemfokea mwanzisha thread eti ''awe na heshima na adabu'' baada ya kuanzisha thread ya kuonya jinsi kulivyo na utapeli kwenye hiyo site! Hapa umeonyesha tatizo kubwa. Msitu una mbwa mwitu ametokea msamaria anawaonya wanaokatiza msitu ule wawe waangalifu wewe badala ya kushukuru unafoka? Umekuwa mbwa mwitu? Ni kweli kwenye internet kuna utapeli wa kina aina na anapotokea mtu akatahadharisha ni vizuri kwani kuna wageni wengi ambao hawajui. Wewe kama unajua na umeshafanya manunuzi sijui ebay nk usikataze wengine kujulishwa! Halafu mwanzisha thread hakusema wamiliki wa mtandao ndio wezi bali ameelezea kuwa kuna wauzaji wanaweza kuwa matapeli. Wewe ni nani mpaka ufoke? Ebo!
Kumbe kuna na wake? Nipe website yaoGari atanunuliwa lingine, jamaa aliwahi kutapeliwa mke,yaani mahari alilipa yeye ila kuoa akaoa mwingine!