Huu ndio usaliti halisi

VIVIANET

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2015
Posts
2,129
Reaction score
2,922
Neno usaliti limekuwa likitumika vibaya, na kupoteza maana halisi ya neno usaliti.

Maana hasa ya neno usaliti ni kwenda kinyume na makubaliano ya jamii au kundi fulani. Neno usaliti pia linaweza kumaanisha kutokuwa mwaminifu kwa makubaliano.

Huyu ndie msaliti halisi, tulikubaliana wote kwa pamoja kuwa na katiba mpya inayotokana na maoni ya wananchi, mchakato ulifanywa na tume iliundwa, maoni ya wananchi yakakusanywa kutoka pande mbili za muungano wa jamuhuri ya Tanzania. Ikafikia kiwango cha kuwa na bunge maalumu hadi mijala ilipoisha na katiba pendekezwa ikaandikwa.

Msaliti halisi akatokea akaamua kuwasaliti watanzania wote, bila kujali muda uliotumika na gharama kubwa ya kuendesha zoezi hilo, msaliti ametusaliti watanzania na kutuona wananchi hatufahi, na hata kiongozi aliyeridhia mchakato kuwa hafahi. Huyu ndio msaliti halisi
 
Mabilioni yote yale kupotea bure?
 
Yule mzee aliyetangulia mbele za haki ndiye msaliti namba moja
 
Napaza sauti kuu kwa kusema ee mungu nakuomba kwa sauti kuu kabisa iliyo shiba huyu SAMWELI SITTA anastahili adhabu kali sana huko aliko kama adhabu zipo, lakini naomba atandikwe viboko kila siku asubuhi na jioni viboko 54
Dhambi aliyo watendea watanzania nikubwa mno.

Lakini pia ee mungu naomba aliyekuwa Mh rais wa awamu hiyo naye akifika huko apewe adhabu kali mara 1000 ya hiyo ya SITTA maana huyu ndiye msaliti nambari one na msdiye aliye iangamiza tanzania nankuifanya ikose katiba bora kabisa ,ameni!!
 
Sala yako imebakisha genge.
Je wale wabunge wa bunge la katiba waliokodishwa ili kuvuruga kwa makusudi kwa njia ya vijembe.
Tena watu hao ni wasomi na akili zao, lakini walijifyetua kwa makusudi na kukojolea "maoni pendekezwa ya Warioba", wao unawaombea wakifa waje kulambishwa chai ya viboko vingapivingapi kila siku?
Ninataka wasikie kabisa, maana bado wapo.
 
Kuna mtu Ana kiloba upande wa pili wa barabara sijui cha nini anakuangalia kweli sijui kwa nini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…