Israeli ya Kale ni jina la watu au taifa walioitwa taifa teule katika
Tanakh au
Biblia ya Kiebrania (kwa hiyo pia katika
Agano la Kale lililo sehemu ya kwanza ya
Biblia ya Kikristo.
Kihistoria waliishi katika nchi iliyoitwa
Kanaani, halafu
Israeli (baadaye pia
Palestina) kuanzia mnamo
1200 KK hadi mnamo mwaka
70 BK Waroma wa Kale walipovamia na kuharibu
Yerusalemu, ambao tena mwaka
135 waliwafukuza wote kutoka nchi yao.
Wenyeji walijiita mwanzoni
Wanaisraeli na baadaye pia
Wayahudi.
Historia ya Israeli ya Kale inaanza tangu kupatikana kwa taifa hilo katika nchi yake inayoitwa Israeli. Kufuatana na masimulizi ya Agano la Kale taifa la Israeli lilianzishwa na Wanaisraeli waliotoka Misri chini ya uongozi wa Musa na kuvamia Kanaani mnamo mwaka 1200 KK chini ya Yoshua.
Wataalamu wengine wa kisasa wanaona ya kwamba taifa lilitokea hasa ndani ya nchi kwa kuungana kwa vikundi mbalimbali.
Muungano huo wa vikundi na makabila ukawa taifa na kuunda ufalme wa kwanza wa Israeli wakati wa mfalme Sauli aliyefuatwa na Daudi na mwanae Suleimani.
Baada ya kifo cha Suleimani likatokea farakano na jina la "Israeli" likatumiwa na ufalme wa kaskazini, wakati mji mkuu wa kale Yerusalemu ukaendelea kama mji mkuu wa ufalme wa Yuda.
Falme zote mbili zilishindwa katika vita na kuanzia mwaka 587 KK hapakuwa tena na dola la kujitegemea, bali eneo lilikuwa chini ya falme mbalimbali kama vile Babiloni, Uajemi na Ugiriki wa Kale.
Lakini harakati za Wamakabayo za kurudisha uhuru uliweza kuwafukuza Wagiriki na kuanzisha ufalme wa Kiyahudi kati ya 140 KK hadi 4 KK.
Hata hivyo kuanzia mwaka 63 KK ufalme huo uliwekwa chini ya ulinzi wa Dola la Roma na polepole kugawiwa na hatimaye kuwa jimbo la Kiroma (tangu 70 BK).
Maangamizi ya Yerusalemu mwaka 70 BK huhesabiwa kama mwisho wa Israeli ya Kale. Wataalamu wengine wanaona tayari uvamizi wa mji wa 587 KK na Wababeli kama mwisho wa kipindi hiki na kuangalia kipindi kati ya 587 KK hadi 70 BK kama kipindi kipya.
Wakati wa
Agano Jipya,
mji wa Yerusalemu, pamoja na nchi ya Israeli/Palestina, vilikuwa chini ya Dola la Roma, ambalo lilitawala maeneo yote yanayozunguka
bahari ya
Mediteranea. Mkuu wa Dola alikuwa na cheo cha "
Kaisari" akikaa mjini
Roma (
Italia).
Waroma walidai
utiifu na
kodi za mataifa na makabila yote yaliyokuwa chini yao. Lakini hawakuwa na neno juu ya
utamaduni na
dini za nchi hizo.
Utawala wa Kiroma ulirahisisha
biashara na
uchumi pamoja na
mawasiliano katika maeneo haya yote. Waroma hawakuwa na mitambo ya
injini lakini walikuwa wataalamu wa
uhandisi. Walikuwa hodari sana kujenga
barabara na
nyumba za
ghorofa. Majengo kadhaa waliyoyajenga husimama mpaka leo.
Magofu ya miji yao yanaonekana leo hii kuanzia
Misri na
Algeria hadi
Ujerumani na
Asia.
Wasanii wao walichonga
sanamu za
mawe za kudumu.
Israeli/Palestina ilikuwa na
serikali yake ya Kiyahudi lakini pia na
liwali au
gavana wa Kiroma. Waroma walizima kwa ukali majaribio yote ya kupindua utawala wao. Wayahudi katika Israeli walijaribu mara mbili kuwafukuza Waroma nchini: miaka
66-
73 na
135 BK. Kila safari Waroma walilipiza
kisasi, wakichoma
moto miji na vijiji na kuwafanya wananchi kuwa
watumwa au kuwaua kabisa.
Na mkurugenzi wa mashirika