HUU NDIO MWENDO KASI.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
4,972
2,000
MWENDO KASI.

1)ni vu zaidi ya honda,hivyo ndivyo wavyoona.
Vitambi vya zidi konda,vinakufa vya kunona.
Ndo tunda walilopanda,kuleni acha kununa.
Huo ndio mwendo kasi,karibia utazima.

2)sasa ngumu kuuliza,dereva huyu ni vipi.
Japo leta mza mza,utajwa geuzwa kapi.
Ndivyo wao wanawaza,hivi tunaenda wapi.
Huo ndio mwendo kasi,karibia utazima.

3)hata hadi kutamka,nako ni mwendo wa vuu.
Viunzi vinafumuka,wakijua wapo juu
Ngoja tuje kufunguka,waone tutavyo vuu.
Huo ndio mwendo kasi,karibia utazima.

4)wanatufungia ndani,ili wayatende yao.
Hawajui ya kijani,itanyaukia kwao.
Wasubiria mwakani,lije kufa gari lao.
Huo ndio mwendo kasi,karibia utazima.

5)wanakaba na manati,iliosukwa na wote.
Ila zi zao kamati,ziwe kwa nyakati zote.
Hata bila ya tamati,wameka vikao vyote.
Huo ndio mwendo kasi,karibia utazima.

6)bila hata helementi,makorongo yamezidi.
Itayayuka sementi,utaisha ukaidi.
Si mabini na mabinti,watajwa pakws magadi.
Huo ndio mwendo kasi,karibia utazima.

Shairi=MWENDO KASI.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160.
iddyallyninga@gmail.com
Facebook page=Idd ninga mashair.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom