Apo zamani kulikuwa na mwana mama mmoja aitwaye TUNDO,huyu mama hakubahatika kupata mtoto,hali iliyofanya ndoa yake kuwa matatani,kwani ndugu wa mume wake hawakumpenda kabisa, sababu ilikuwa ni ugumba wake.Tundo aliahangaika sana ili apate mtoto,baadae tundo akaamua kwenda kwa waganga,katika hangaika yake akakutana na mganga mmoja nchini Congo,mganga akampa dawa tundo za kutosha.Kweli dawa zile zilizaa matunda kwani mda mfupi tundo akapata ujauzito hatimaye akajifungua mtoto wa kiume akamwaita SINDUNA..Maajabu ya mtoto yule baada ya kuzaliwa alikuwa na meno yote kama mtu mzima,tundo alifurah sana kwani aliamini mganga amemsaidia.Siku moja tundo alikuw akimnyonyesha mtoto wake,ghafla yule mtoto akamng'ata kwenye ziwa,mwili wa tundo ukapoa wote upande mmoja,tatizo lilikuwa kubwa kwani mwili wa tundo ulianza kubadilika,ngozi yake ikawa kama gamba la nyoka.Siku moja ndugu wa tundo wakamtembelea ndugu yao na kumkuta tundo kwenye hali mbaya,walilia sana na kumwambia tundo waende kwa mchungaji ili wakamfanyie maombi.Tundo aliondoka na mtoto wake hadi kanisani,mchungaji alipomuona tundo na mtoto wake,mchungaji akamuita tundo mbele ya madhabahu,akamuuliza tundo umebeba nini mgongoni mwako??,tundo akajibu kwa kujiamini nimebeba mtoto,mchungaji akamwambia tundo amshushe yule mtoto chini,tundo akafanya hivyo.mchungaji akaomba sana mara yule mtoto akageuka na kuwa CHATU mkubwa,watu wote wakakimbia,mchungaji akamwambia tundo njoo umbebe mtoto wako,guess what's next???,hii nyimbo ni kali sana na inafundisha,inaitwa MAAMUZI,imeimbwa na BAHATI BUKUKU...
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums