Huu mchakato wa katiba "mpya" umeshanichanganya! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu mchakato wa katiba "mpya" umeshanichanganya!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwananchit, Nov 18, 2011.

 1. m

  mwananchit Senior Member

  #1
  Nov 18, 2011
  Joined: Oct 13, 2008
  Messages: 144
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kuna mambo matatu (3) siyaelewi kuhusu huu mchakato wa kupata katiba mpya.

  1. Suala la katiba mpya lilikuwa siyo agenda ya ccm na wala halikuwa kwenye ilani yake ya uchaguzi wa mwaka jana, na hata waziri wa sheria pamoja na mwanasheria mkuu wa serikali walipata kutoa maoni ya kukatisha tamaa kwa wale waliokuwa wanadai katiba mpya. Cha ajabu ni kwamba walewale waliokuwa hawaitaki katiba mpya, leo ndio wako kimbelembele wakitaka ipatikane haraka iwezekanavyo-hawataki hata kupoteza muda kwa kutupa sisi wananchi muda wa kupitia huo muswada wa uundwaji wa tume na bunge la katiba! Hivi hii haraka ambayo hawakuwa nayo wakati wanaandaa ilani yao ya uchaguzi sasa wameipata wapi?

  2. Hivi Celina Kombani aliwasilisha bungeni muswada upi, wa katiba au wa Tundu Lissu? Naona huyu jamaa anajadiliwa kwa nguvu kuliko katiba, au na yeye ameshaunganishwa na wale walio juu ya katiba?

  3. Hivi huyu jamaa aliyesimamia vyema ugawaji wa viwanda vyetu, benki yetu ya NBC na bureau de change yake na hatimae akashushia na rada vilivyomwezesha kuwa na akiba ya vijisenti huko ughaibuni huku akiendelea kushikilia uongoji wa kisisasa katika nchi yetu iliyojaa amani tele, na hayo yote yakiwezekana kutokana na katiba mbovu tuliyonayo, anapochangia muswada wa katiba maana yake ni nini kama siyo kutaka hii katiba mbovu tuliyonayo iboreshwe kwa kufanywa mbovu zaidi ili aendelee kupeta?

  Jamani naomba mwenye majibu ya hizo hoja anielimishe.
   
Loading...