‘Hustle’ yako ya kwanza ulilipwa Shilingi ngapi?

T_Dangote

Member
Joined
Apr 23, 2019
Posts
23
Reaction score
28
HUSTLE yako ya Kwanza ulilipwa Pesa ngapi?? taja tuone vile wengi tumetoka mbali!
 
270,000 kama teacher wa advance mathematics, vipindi 4 kwa wiki. Hii nilidumu nayo kwa miezi minne. Kisha nikapata safari kama research assistant kwa Prof mmoja wa SUA. 400,000 kwa wiki. Baada ya hapo nikapata permanent Job .....
 
Nililipwa laki tatu na nusu na elfu tano ya nauli kila siku. Cha ajabu kazi zilizofuata zilikuwa zinalingana au chini ya hapo
 
180,000/= ukitoa makato ya NSSF inabakia 162,000/=[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] na hyo ni kwa mwezi!!
 
laki 1, ila dili za kanjanja inaenda hadi laki 5-7
 
Elfu thelathini kwa siku, kula na kulala free.. kwa miezi minne
 
elfu 8 per day,saidia fundi.tulikua tunajenga nyumba ya ghorofa ya kibopa flani hivi kule moshi. so sisi tukawa ndo wabeba zege..hiyo ilikua 2009.
 
Milion 800 nikadhulumiwa zote.. hela za deal ya petrol..

Deal ya pili nilifoji doc nikapewa tender ya ujenzi wa daraja kama injinia kumbe nimeishia form 4 na ziro nzuri tu.. Nikapewa hela na gari na dereva wa kuniendesha nikapiga zangu Mil 50..
 
6500 ndio ilikuwa ni kazi yangu ya kwanza ofisini kwangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…