MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,997
Uliwafanya hasa wapinzani wa CCM wakae kwenye Television zao wakisubiri Katibu Mkuu wa CCM, Kinana atasema neno kuhusu ‘’kukamatwa kwako’’ kumbe ulitaka tu waangalie kilichokuwa kinaendelea kwenye Mkutano Mkuu wa CCM.
Television za kitaifa na Radio zote zimeonyesha matangazo mubashara ya Mkutano wenu kutokana na ‘’hamu’’ mliyoichagiza hasa wakati ukiongea na waandishi wa habari kuhusu ‘’kadhia ya kukamatwa’’ na polisi.
Hata Mkutano Mkuu ulipomaliza ulihojiwa na kutoa maelezo ambayo wapinzani ninaamini hawakupenda kuyasikia!
Mungu anawaona jinsi mnavyowasumbua wapinzani nchini kwa kuwajaza upepo wa kisiasa ambao baadaye unatoka haraka na kuacha matumbo yao wazi (back to square one).
Mnajua wapinzani wenu wanapenda kusikia habari za mapambano na mvurugano ndani ya CCM na kwa kufahamu hivyo huwa mnatengeneza mazingira ya kuwafanya wapinzani wenu wafatilie kinachoendelea ndani ya CCM. Kwa maana nyingine mnawafanya wapinzani wafanye siasa za matukio.
Kuna magazeti kama Tanzania Daima na MwanaHalisi hayakuishia kujaa upepo tu bali yamefikia mpaka kuweka vichwa vya habari vinavyosema, ‘’CCM yapasuka’’.
Kuna watu watapoteza muda wakisubiri huo mpasuko!
Nyie CCM mna propaganda za ajabu kweli! Mwogopeni Mwenyezi Mungu!
Watendeeni haki wapinzani nchini na sio kuwajaza upepo wa kisiasa na baadaye kuwaacha matumbo wazi.
VIDEO: Hussein Bashe akihojiwa kuhusu habari ya kukamatwa.
VIDEO: Hussein Bashe akihojiwa baada ya Mkutano Mkuu wa CCM.