Husein Massanza: Ukimtaka Sowah njoo na Tsh. Bilioni 2.6 Singida BS

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,498
Klabu ya Singida Black Stars kupitia kwa Afisa Habari wake Husein Massanza imesema mshambuliaji hakuna timu Tanzania yenye uwezo wa kumnunua mshambuliaji wao Jonathan Sowah na kubainisha kuwa kama kuna timu inajiweza ije mezani na kitita cha Tsh bilioni 2.6.

"Ikitokea klabu inakuja inataka kumnunua (Jonathan Sowah), inaona inajiweza weza, dau mezani ni Dola za Kimarekani milioni 1 (Tsh. bilioni 2.6). Tunathubutu na kujiamini tukisema kwamba kwa Tanzania hakuna klabu yenye uwezo wa kutoa bilioni 2.6." Massanza

Hata hivyo, inaripotiwa kuwa Simba SC tayari wamemfuata mchezaji huyo na project nzuri, na kijana amekubali bila kusuasua. Vyanzo vimedokeza kuwa dili limekamilika, na sasa ni rasmi kwamba msimu ujao Sowah atavaa jezi ya Mnyama.

Chanzo: UFM
 
Mkuuu umekosa Habari au unataka kujaza serva za Jamii Forum bila sababu za Msingi?????

Kweli kuna haja ya kuanza kumukuu kauli za Hawa watu wa habari wa timu za Ligi kuu Tsnzania????

Binafsi naona ni kujidhalilisha tu.
Hao maafisa habari ni wapumbavu.
Wazushi, wajinga, wana mizaha nk
 
Klabu ya Singida Black Stars kupitia kwa Afisa Habari wake Husein Massanza imesema mshambuliaji hakuna timu Tanzania yenye uwezo wa kumnunua mshambuliaji wao Jonathan Sowah na kubainisha kuwa kama kuna timu inajiweza ije mezani na kitita cha Tsh bilioni 2.6.

"Ikitokea klabu inakuja inataka kumnunua (Jonathan Sowah), inaona inajiweza weza, dau mezani ni Dola za Kimarekani milioni 1 (Tsh. bilioni 2.6). Tunathubutu na kujiamini tukisema kwamba kwa Tanzania hakuna klabu yenye uwezo wa kutoa bilioni 2.6." Massanza

Hata hivyo, inaripotiwa kuwa Simba SC tayari wamemfuata mchezaji huyo na project nzuri, na kijana amekubali bila kusuasua. Vyanzo vimedokeza kuwa dili limekamilika, na sasa ni rasmi kwamba msimu ujao Sowah atavaa jezi ya Mnyama.

View attachment 3418461
Chanzo: UFM
Labda wawauzie Yanga......
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom