Samahani, naomba nichangie kwa namna tofauti ...
Kwa sehemu, kuna ukweli kuwa wanandoa (husband & wife) wanaoishi pamoja, kila mtu anaweza kuwa kikwazo kwa mwenzio mpaka kufikia hatua ya kumpa pressure au ugonjwa wa moyo kwa kufanyiana tabia zisizo nzuri. Hii imesababisha mahusiano ya kindoa yaonekane kana kwamba ni mabaya na ya kukatisha tamaa. Lakini ukweli ni kwamba, wanandoa (Husband na wife) hawana matatizo makubwa ya kiasi hicho kama wengi wanavyofikiri, ila wachache wenye matatizo, yamekuwa wazi na kuifanya ndoa ionekane kama shimo la mateso!
Kikubwa ni kuwashauri Husband na wife wawe na upendo wa dhati, wakishirikiana, kushauriana na kusaidiana katika shida na raha, huku wakivunja ukimya juu ya suala zima la rusha roho kama haliendi vzr ndani ya mahusiano yao na namna ya kutatua tatizo hilo.
Hii itatusaidia kuepukana na haya ambayo ndugu yangu Ndallo ameyaandika.
Thank you Ndallo kwa kutukumbusha hayo.