shikwashikwa
Senior Member
- Jun 5, 2015
- 188
- 46
Wasalamu wana jamvi,
Ninae mpenzi ambaye miezi 3 mbele panapo majaliwa tutafunga ndoa, nashukuru MUNGU kwani ni mwema kwa kunipa mwenza panapo majaliwa. Huyu mke wangu mtarajiwa ni mpole na mwenye huruma sana anarafiki yake chakaramu kidogo kanizoea lakini hatuna utani nae, anampenda sana rafiki yake mke wangu mtarajiwa.
Kwani katika historia ya urafiki wao kasaidiwa mambo mengi sana sana moja la mfano ni kulipiwa Ada ya chuo mwaka mmoja baada ya ndugu zake kukwama kiuchumi hilo ni moja tu lakini yapo mengi mengi kwa mfano ameshaishi nae mwaka na nusu kwake kula, kulala na kila kitu juu ya rafiki yake. Sasa Jana nilipigiwa simu kuwa anaomba tukutane tuongee nikaona sio mbaya shemu wangu wa nguvu tena nikamuelekeza sehemu huwa pana michemsho mbali mbali, punde akawa amefika.
Baada ya salamu na maongezi ya hapa na pale akasema tafadhali shemu naomba usimsaliti mke wangu mtarajiwa ataumia sana hata kama unafikiria kuwa na mchepuko ni bora hata ukaniambia mimi kuliko kutoka na wanawake wa huko.
Nikamuuliza kwani vipi? Akaniambia eti kuna mtu anapeleka habari kwa wife to be kuwa mimi natoka na wafanyakazi wenzangu na huyo jamaa aliwahi kumtaka akamtolea nje.
Nikakataa na kumuuliza kwani nikitoka na wewe nitakuwa sijamsariti? Akanijibu bora mimi sitakuwa na wivu na nitakuwa na heshima.
Nimefikiria nikaona sababu mbili
1~Nategwa
2~Huyu anahuruma kwa shosti wake lakini hajui kama ndio anamfanyia ukatili.
Nimepanga leo nikutane na mke wangu na nimueleze yote haya, sijui nitakuwa nimekosea?
Naombeni mnishauri kistaarabu
Asante