voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,553
- 11,885
Kuna kundi la "WAHUNI WA KISIASA" ambalo limeibuka na linajijenga kila uchao nchini.
Kundi hili linapatikana kwenye Jamii yetu na hasa hasa kwenye vyama viwili maarufu vya Siasa vya Chadema na CCM.
PolePole, Bashiru Magufuli, Ndugai, Sabaya,
Makonda, Mnyeti na sasa Mdee & Company ni baadhi ya wahanga wa kundi hili.
Kwao yeyote atakaekuwa aliwaza tofauti na mitizamo yao,au
Alichukua hatua zilizokomesha ulaji wao kimfumo.
Basi huyo ni adui wao na hastahili kuishi kwa amani popote pale alipo,kwa kuwa tu,amehatarisha au kuzuia maslahi yao binafsi.
Mtu au watu hao watapewa majina yote mabaya ikiwemo Usaliti,Uuwaji au Udikteta nk.
Wataandamwa kimfumo na kuchafuliwa kimfumo mpaka pale yananapowakuta mabaya yoyote na kuwaweka pembeni ili kupisha wenye malengo yao ovu watimize kile walichokuwa wakikifanya hapo awali kama kawaida.
Imefikia hatua tunaona kule CCM wakiugeuza mkutano mkuu wao wa chama kuwa sehemu ya kupongezana dhidi ya kiongozi aliyetangulia kwenye haki,kwa kupeana majina ya Walamba Asali.
Tunawaona wa huku Chadema nao wakifikia mahali wakawakodishia wafuasi wao usafiri na Posho juu,ili tu wafike mahakamani kumzomea yule waliyemuona kama kizingiti kwenye siasa zao jimboni kwa Mwenyekiti wao Mbowe.
Na ilipotolewa hukumu ya miaka 30 jela kwa mbaya wao Sabaya.
Walishindwa kuficha furaha yao mitandaoni mpaka kwenye viti moto na bia baridi huko mitaani.
Hali ilikuwa hivyohivyo kwa Spika Mstaafu Job Yustino Ndugai hadi alipotenguliwa na kupisha kiti cha uspika wa bunge la JMT.
Baadae wakahamishia mashambulizi upande wa pili kwa mbaya wao mwingine Makonda.
Si kwenye magazeti,mitandaoni,Club house na kila nyenzo waliyoweza. Kazi ilikuwa moja tu...
Komoa Makonda!
lakini bahati mbaya kwao na nzuri kwa Makonda.bado Dua lao halijasikilizwa.
Ila ghafla likajitokeza pigo.....Sabaya Mbaya akashinda rufaa mahakamani na kuachiwa huru,huku akiendelea kuwa mahabusu kusubiri hukumu ya kesi ingine hapo Mei 30.
Salaaleh....povu likaanza upya kuanzia Club House mpaka twitter na humu JF tumeona hasira ilivyokuwa ikiendelea.
Lakini ilipokuja suala la waliokuwa wanachama maarufu Chadema kabla ya kufukuzwa kwa kupingana na maelekezo ya chama chao.
Na hatimae muda wa rufaa zao mbele ya Halmashauri Kuu ya chama chao kuwadia.
Mashambulizi yote kwa Sabaya na Makonda yakaadimika au kukoma kabisa mitandaoni na kwingineko.
Badala yake tukaona yamehamishiwa kwa hawa wabunge 19 wa chadema pamoja na Spika mstaafu Yustino Job Ndugai.
Maamuzi yakatoka na Halima & Company wakafukuzwa rasmi kutoka Chadema kwenye kikao kilichoisha usiku wa manane pale Mlimani City.
Asubuhi kulikucha na Sherehe mitandaoni mpaka huko Club Houses na Magazeti yale yaliyoko chini ya makada wa chadema ambayo ni
"Tanzania Daima"
la Mwenyekiti Mbowe.
Na lile aliloajiriwa
Said Kubenea kwa sasa "Raia Mwema".
Na leo furaha imegeuka ghafla kuwa povu........
Pale Spika Tulia Akson Mwansasu,alipotangaza rasmi bungeni Dodoma.
Maamuzi ya kusubiri mhimili wa mahakama Kuu ukamilishe Hukumu ya kesi ya msingi,
iliyofunguliwa na wabunge hao kupinga kuvuliwa kwao uanachama.
Huku wakiitumia mahakama hiyo hiyo kuweka zuio la wao kuvuliwa ubunge mpaka shauri la msingi litakapoamuliwa na mahakama.
Saa hii humu tunaona makombora mapya kutoka kila kona ya chadema kuelekezwa kwa Spika. Mengine yakiwa mashambulizi binafsi kwake.
Na mengine yakirushwa kwa serikali ya CCM.
Lakini wanaenda mbali kwa kumtaka Mbowe amuombe Rais Samia kumlazimisha Spika kuwatimua bungeni bila kusubiri hatua za kisheria kwa mujibu wa katiba ya JMT.
Hapa tunaona lengo sio kufukuzwa uanachama kwa hao 19 tu.
Bali lengo ni kuwaona wakiteseka mtaani kama hawa wengine.
Waliokubali kufuata maelekezo,wakiwemo madiwani kibao waliokuwa wameshinda kwenye uchaguzi mkuu wa 2020.
Na kwa upande mwingine tumesikia kuna wateule wapendwa wengine 19 waliokuwa tayari wameandaliwa huo ulaji pindi hao kina Mdee watakapoachia ngazi.
Je hizi siasa za kukomoana zitatufikisha hadi wapi kama taifa??