Hapana. Napenda sana kukosolewa. Ila lazima tukubali kuna watu hawana mamlaka ya kimaadili leo kuzungumza hivi leo na jana vile.
Kwa sasa tusiangalie anafanya kwa sababu ya nani, madhali anachosema ni sahihi, anatetea upamde sahihi, ni ukweli uliokuwa wazi kabisa sasa nchi inaendeshwa kihuni zaidi kuliko nyakati zilizopita, taifa letu linahitaji mabadiliko makubwa, lakini hata chama tawala ndani yake wanahitaji marekebisho makubwa.
HAIWEZEKANI mtu atekwe hadharani,auawe kisha raisi aseme kifo ni kifo tu.
Mpina kaonesha ufisadi wa bashe sio kwa chuki, kaonesha jinsi gani wanahitaji maendeleo, anatolewa madarakani, sasa kama nchi hatuwezi emda hivi.
Serikali gani haitaki kuambiwa, haitaki kukosolewa,
Yenyewe inataka kusifiwa tu, hata sifa za kijinga.
Deni la taifa linapaa lakini miundombinu tqnzania ni hovyo.
Watu wachota mihela huko kwa vimemo tu..
Wacache wanajirundikia mali.
Mkuu wa wilaya kwenda kuishi hotelini, sio hoteli chumba 100k..
Tukiongea tunaambiwa tuhamie burundi, kweli... Taifa hili ni la kwao pekee yao?