Humphrey Polepole: Rais Magufuli anatekeleza Katiba Mpya

Salaam Wanajamvi.

Ni maneno ambayo yameaandikwa kwenye Gazeti la Mwananchi Januari 04,2017, kuwa eti Rais Magufuli anatekeleza Katiba Mpya.

Polepole anataka kutuaminisha kuwa hakuna haja ya kuwa na Katiba Mpya kwa mwelekeo wake. Inavyoonekana tayari anaanza kusahau hata kile alicho ahidi hivi majuzi kuwa hatakaa kusaliti kile alichokuwa amesimamia kwenye suala la Katiba. Kweli Madaraka matamu, naam ni matamu zaidi ya asali.

Alianza Mzee Warioba Kusaliti misimamo yake juu ya Katiba Mpya kwa kuendelea kuwapa Nafasi waliyoharibu Katiba Mpya na sasa Polepole naye anaenda kivitendo zaidi. Kwa mwendo huu ni dhahiri Kupata katiba Mpya kwa Kutumia Makada wa CCM ambao ni wateule wa Rais ni vigumu, vinginevyo tuamke wenyewe kupaza sauti wananchi wenyewe.


By Elias Msuya, Mwananchi emsuya@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema Serikali ya chama hicho inayatekeleza maoni yaliyotolewa na wananchi wakati wa mchakato wa Katiba Mpya kwa kuyafanyia majaribio.

Akizungumza katika kipindi cha Mada Moto kinachorushwa na televisheni ya Channel Ten, Polepole amesema mchakato wa kupata Katiba Mpya ni mgumu kuuendeleza kwa sasa hadi hapo Rais John Magufuli atakapoinyoosha nchi.

Mchakato wa Katiba Mpya ulizinduliwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwishoni mwa mwaka 2011 alipounda Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba na Polepole akiwa mmoja wa wajumbe.

Hata hivyo, mchakato huo uliishia kwenye Bunge Maalumu la Katiba ambalo licha ya kupitisha Katiba Inayopendekezwa ambayo haijapigiwa kura ya maoni hadi leo, baadhi ya vyama vya upinzani vilijitoa na kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).


Ahsanteni.
Afadhali mchawi Nape kuliko mnafiki polepole.
 
Spot on. Magufuli akiongoza katika hilo. Wanawaonea watumishi wa kada za kati na chini tu; huku Magufuli na wateule wake wakila kuku kwa mrija.
Wanafuta posho za Watumishi huku wao wanakula vizuri. Huoni Presidaa anazidi kutoka Kitambi. Uonevu kabisa huu. Anasema waishi kwa Mishahara yao, je wao wanaishi kwa mishahara?
 
Back
Top Bottom