Humphrey Polepole aeleza mikakati yake baada ya kukabidhiwa chama

McCain

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2016
Posts
1,168
Reaction score
517
Humphrey Polepole aeleza mikakati yake baada ya kukabidhiwa ofisi na Nape Nnauye

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole amesema atahakikisha chama hicho kinakuwa ni cha wanyonge na kuendelea kuwa kimbilio la wasio na sauti.

Polepole ametoa kauli hiyo leo wakati akikabidhiwa rasmi ofisi na Katibu anayemaliza muda wake Nape Nnauye katika ofisi ndogo za Makao Makuu ya chama hicho Lumumba jijini Dar es Salaam.

Polepole alisema kwa misingi ya chama hicho imejengwa kuwasaidia na kuwa tete wanyongo hivyo katika muda wake wa uongozi atahakikisha chama kinasimama katima misingi hiyo ya kuanzishwa kwake.

“Msingi wa chama chetu ni utetezi wa wanyonge, tutahakikisha kinaendelea kuwa kimbilio la wasio na sauti,” alisema Polepole.

Aidha, katibu huyo alisema kuwa katika kutekeleza majukumu yake aliyokabidhiwa leo na mtangulizi wake, atahakikisha anajikita zaidi katika kazi za itikadi zaidi kuliko uenezi kwa kuwa itikadi ndiyo inayokibeba chama.

Polepole alitumia muda huo kumshukuru Nape Nnauye anayemaliza muda wake na kusema kuwa ni kiongozi imara na kuwa katika muda wake aliweza kuitumikia vyema nafasi yake. Lakini pia alisema japo anamaliza muda wake, lakini atakuwa akimuhitaji mara kwa mara kwa ajili ya ushauri na mambo mengine.

Wakati huo huo, Polepole amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Dkt John Pombe Magufuli na Halmashauri Kuu ku kumwamini na kumpa majukumu hayo makuwa.

Chanzo:
Mpekuzi
 
uwiz

Visit website

View attachment 446568
uwizi mtupu kama kuna awamu masikini wanatembea na kamba shingoni ni huu,eti chama cha wanyonge! kweli mnawanyonga kikwelikweli
 
Ccm toka lini ikawa lafiki wawanyonge huu niuongo ulikomaa wangekuwa lafiki wawanyonge wasingekua wanakwapua malizauma..mabilioni walioiba mwaka juzi bado tunayakumbuka mpakaleo nawalioiba wako mtaani wanakula bata nafamilia zao..sasanajiuliza hiyomahakama yamafisadi inafanya kazigani au nimahakama ya wapinzani ..maana mafisada yakomengi lkn hata moja halijakamatwa
 
Hata hivyo,Mimi siyo mnyonge nikiwa hapa Tanzania,labda atawatetea ninyi huko
 
Msingi wa chama chetu ni utetezi wa wanyonge, tutahakikisha kinaendelea kuwa kimbilio la wasio na sauti,” alisema Polepole.
Point tupu.
tz}ccm.gif
 
Wanataka kuendelea kuwafanya watanzania wanyonge milele,shame!
 
Wanyonge wanaumizwa kwa uhuni uliofanywa na watu wa chama chake huyu kwa kuingia mkenge wa makusudi wa mkataba na IPTL. Hela zinalipwa kwa mabilioni lakini umeme hadithi.
Hebu amstue mwenyekiti wake kuhusiana na hili maana amelikalia kimya kama mwenyekiti aliyepita. Au hili lina mizizi mirefu iliyoenda chini sana kwenye mhimili mkuu?
 
Chama cha ccm, chama cha kuteka watu na kubambikizia makesi tu!!
 
Humphrey Polepole aeleza mikakati yake baada ya kukabidhiwa ofisi na Nape Nnauye

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole amesema atahakikisha chama hicho kinakuwa ni cha wanyonge na kuendelea kuwa kimbilio la wasio na sauti.

Polepole ametoa kauli hiyo leo wakati akikabidhiwa rasmi ofisi na Katibu anayemaliza muda wake Nape Nnauye katika ofisi ndogo za Makao Makuu ya chama hicho Lumumba jijini Dar es Salaam.

Polepole alisema kwa misingi ya chama hicho imejengwa kuwasaidia na kuwa tete wanyongo hivyo katika muda wake wa uongozi atahakikisha chama kinasimama katima misingi hiyo ya kuanzishwa kwake.

“Msingi wa chama chetu ni utetezi wa wanyonge, tutahakikisha kinaendelea kuwa kimbilio la wasio na sauti,” alisema Polepole.

Aidha, katibu huyo alisema kuwa katika kutekeleza majukumu yake aliyokabidhiwa leo na mtangulizi wake, atahakikisha anajikita zaidi katika kazi za itikadi zaidi kuliko uenezi kwa kuwa itikadi ndiyo inayokibeba chama.

Polepole alitumia muda huo kumshukuru Nape Nnauye anayemaliza muda wake na kusema kuwa ni kiongozi imara na kuwa katika muda wake aliweza kuitumikia vyema nafasi yake. Lakini pia alisema japo anamaliza muda wake, lakini atakuwa akimuhitaji mara kwa mara kwa ajili ya ushauri na mambo mengine.

Wakati huo huo, Polepole amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Dkt John Pombe Magufuli na Halmashauri Kuu ku kumwamini na kumpa majukumu hayo makuwa.

Chanzo:
Mpekuzi
Natamani wanafalsafa vijana kama hawa wawe wengi katika chama. Baba wa Taifa aliimarisha chama cha TANU kwa kuelimisha wananchi Itikadi (Ideology) ya TANU,na walimwelewa. Big up !
 
Back
Top Bottom