Hukumu ya Lwakatare Bukoba Vipi?

Mahakama yamwachia huru kiongozi wa upinzani
Lwakatare aachiwa huru

Na Lilian Lugakingira, Bukoba


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kagera imemwachia huru Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Wilfred Lwakatale, katika shtaka lililokuwa likimkabili la kumshambulia na kumjeruhi Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Renatus Mutabuzi, kwa sharti la kutotenda kosa lolote la jinai ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.


Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu wa Mkazi wa mahakama hiyo, Cleophace Waane, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka na kwa kuzingatia maombi ya wakili wa mshtakiwa huyo, Twaha Tasilima, yaliyotolewa kabla ya hukumu hiyo kutolewa.


Akisoma hukumu hiyo, hakimu Waane alisema kuwa mahakama imeona baadhi ya maombi yaliyoombwa na wakili wa mshtakiwa ambayo aliomba yazingatiwe na mahakama wakati wa kutoa hukumu ni ya muhimu, hivyo kuamua kutoa adhabu ndogo kwa mshtakiwa huyo.


Hakimu huyo alitaja baadhi ya sababu hizo zilizoonekana zina msingi kuwa mshtakiwa hilo ni kosa la kwanza wa mshtakiwa, asili ya kosa alilolitenda, nafasi ya ngazi ya juu aliyonayo katika chama cha CUF, afya ya mshtakiwa na jukumu la kutunza watoto alilonalo.


Alisema kwa kuzingatia sababu hizo mahakama imeona kosa alilofanya mshtakiwa ni dogo na kuamua kumwachia huru kwa masharti ya kutotenda tena kosa lolote la jinai ndani ya kipindi cha mwaka mmoja kuanzia jana.


Awali wakati wa kuwasilisha utetezi wa mteja wake (Lwakatare) kabla ya hukumu kutolewa, Wakili Tasili aliwasilisha maombi nane ambayo ni mstakiwa kutowahi kutenda kosa lolote la jinai, kuwa na familia ya mke mmoja na watoto wanne walio na umri wa chini ya miaka 20, kuwa na jukumu la kulea watoto watano walioachwa na ndugu zake ambao ni marehemu na mshtakiwa kuwa mgonjwa wa kisukari tangu mwaka 1997.


Maombi mengine ni mlalamikaji kukubali mwenyewe kuwa hakuumia na mashahidi kuthibitisha kuwa tendo hilo lilichukua sekunde haikufika hata dakika moja na hakikuwa kipigo bali kushika shati lake na wakati kitendo hicho kinatokea kulikuwa na watu wengi lakini hasababisha madhara kwa watu wengine, ni mtu ambaye alitaarifiwa kushindwa katika uchaguzi akiwa katika kundi la watu wengi, madaraka aliyo nayo mshtakiwa katika chama (Naibu Katibu wa CUF taifa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uratibu ya vyama vinne vya upinzani nchini) na kuwa bado yuko katika umri wa kuzalisha wa miaka 44.


Wakili Tasilima aliiomba mahakama hiyo kuzingatia maombi hayo na kwamba maana endapo itampatia adhabu kubwa mshtakiwa hasa ya kumwondosha nyumbani kwake kwa muda mrefu watoto hao wataumia na pia kwa wadhifa alionao katika chama itamnyima nafasi ya kutotumika jamii katika kuleta maendeleo ya taifa na kupunguza kasi ya ukuaji wa demokrasia ya vyama vingi hapa nchini.


Baada ya utetezi huo mahakama ilitoa hukumu ya kumwachia huru kwa masharti ya kutoenda kosa lolote la jinai ndani kipindi hicho cha miaka miwili. Lwakatare alidaiwa kutenda kosa hilo, Desemba 15, 2005.
 
Manvyo Tumia Jina LWAKATALE Uta zani NCHUNGAJI MAMA LWAKATALE ...hata magazeti Yameuza!!
 
Lwakatare chupuchupu kwenda jela

Habari Zinazoshabihiana
• Lwakatare (CUF) vs Kagasheki (CCM) kortini kesho 09.10.2007 [Soma]
• Pingamizi la Kagasheki dhidi ya Lwakatare kusikilizwa leo 17.10.2007 [Soma]
• Hatima ya Nyari, Banjoo Septemba 14 29.08.2007 [Soma]

*Asamehewa na Hakimu, apewa masharti nafuu
*Alipatikana na hatia ya kumpiga mwandishi ITV

Na Theonestina Juma, Bukoba

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi ya Mkoa wa Kagera mjini hapa, imemwachia huru kwa masharti, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Bw. Wilfred Lwakatare (42), katika kesi iliyokuwa inamkabili ya kupiga mwandishi wa habari.

Hukumu hiyo ya kesi namba 457/2005 ilitolewa jana na Hakimu wa Mahakama hiyo, Bw. Cleophace Wanne, baada ya kupokea na kuridhia utetezi uliotolewa wa wakili wa kijitegemea, Bw. Twaha Tasilima, ambaye alikuwa akimtetea Bw. Lwakatare kabla ya Mahakama kutoa hukumu hiyo.

Ilielezwa katika mahakama hiyo iliyofurika watu wengi kusikiliza hukumu hiyo na Mwendesha Mashitaka wa Polisi Jumanne Ibrahimu kuwa Bw. Lwakatare alitenda kosa hilo la kumpiga mpiga picha wa kituo cha ITV, Bw. Renatus Mutabuzi, Desemba 15 mwaka juzi saa 5 asubuhi katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba.

Hakimu Wanne alisema mahakama inaridhika na utetezi uliowasilishwa na Wakili wa Bw. Lwakatare, kutokana na kile alichoeleza kuwa kitendo alichofanya kilikuwa kidogo na kuwa hakikuweza kumletea madhara mlalamikaji na hasa yakiangaliwa mazingira ambayo tukio hilo lilitokea na watu waliokuwapo wakati huo, hawakuweza kuathirika kwa lolote zaidi ya mtu mmoja ambaye ni mwandishi wa habari.

Hakimu alisema mahakama inamwachia huru mshitakiwa kwa masharti ambayo kwa kipindi cha mwaka mmoja, hatatakiwa kutenda kosa lolote.

Hata hivyo, Wakili wa Bw. Lwakatare, Bw. Tasilima alisema masharti hayo hayataathiri kesi yake ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka juzi kama utarudiwa.

Awali, kabla ya kuanza kutolewa hukumu ya kesi hiyo, Wakili Taslima aliwasilisha maelezo yake ya utetezi juu ya mteja wake, yakiwa ni pamoja na mahakama hiyo kutoa adhabu ndogo kwa mshitakiwa huyo kwa kuangalia mambo muhimu kabla ya hukumu.

Mambo hayo ni pamoja na mshitakiwa kutokuwa na rekodi ya kutenda kosa, ikiwa hilo ni kosa lake la kwanza katika maisha yake na kwamba ana familia ya watoto wanne ambao hawajafikisha miaka 20 na mke, ambao wote wanamtegemea, ikiwa ni pamoja na watoto watano yatima wa kaka na ndugu zake ambao wanamtegemea.

Na hivyo akipewa adhabu kwa kipindi kirefu, itaweza kuwaondosha watoto hao nyumbani kwake.

Hali kadhalika alibainisha kuwa mshitakiwa huyo anasumbuliwa na kisukari kwa kipindi kirefu tangu mwaka 1997 na amekuwa chini ya uangalizi wa daktari, na katika kudhihirisha hilo, Wakili aliwasilisha baadhi ya vyeti vya mteja wake mahakamani hapo, ikiwa ni pamoja na cheti cha Oktoba 15 mwaka huu ambapo alipimwa kisukari kwa mara ya mwisho.

Pia alibainisha, kuwa kama anavyokubali mlalamikaji kuwa hakuumia na katika ushahidi wake mashahidi wake walioaminiwa na makahama hiyo, walidai kuwa kitendo cha kupigwa kwa mwandishi huyo hakikuchukua hata dakika moja, zaidi ya kumkwida shati shingoni.

Mengine ni kuwa tukio hilo lilitokea wakati kuna watu wengi na hivyo hakuweza kuleta madhara yoyote kwa mlalamikaji na ikizingatiwa kuwa ilikuwa ni mara yake ya kwanza kutaarifiwa, kuwa hakushinda katika uchaguzi huo, huku akiwa katikati ya watu angweza kulalamikiwa na watu wengi, lakini haikutokea hivyo, zaidi ya kulalamikiwa na mtu mmoja.

Pia, Bw. Taslima aliiomba mahakama kuangalia wadhifa alionao mshitakiwa huyo katika jamii na Taifa kwa jumla, kwamba ana madaraka makubwa taifani akiwa ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF Taifa, kutokana na hilo, yeye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kuratibu Muungano wa Vyama vya Upinzani nchini na hivyo, kumwondoa kwa muda mrefu katika jamii, itakuwa ni kuinyima nchi nzima mchango wake wa maendeleo ya Taifa.

Pia kutampunguzia kasi ya ukuzaji demokrasia ya vyama vingi nchini na kwamba akiondolewa kwenye uhuru alionao kwa hivi sasa, mchango wake pia utaondolewa katika jamii ya Watanzania.

Hakimu Wanne aliridhika na vipengele vyote vilivyowasilishwa na wakili huyo na hivyo kumwachia huru kwa masharti ya kutotenda kosa lolote.

Wakati huo huo, kesi yake ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi, unaanza kusikilizwa leo na Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, baada ya Jaji Shaaban Lila kutolea uamuzi pingamizi lililowasilishwa na mawakili wa Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki.

Jaji Lila alisema kesi hiyo itaanza kusikilizwa leo kwa upande wa mashahidi wa mlalamikaji kuanza kujieleza.

Aidha, pingamizi lililowasilishwa mahakamani hapo na Wakili wa Kagasheki liliridhiwa na Jaji huyo, ambapo vilibakia vipengele ambavyo viliwasilishwa kwa mara ya kwanza na Wakili wa mlalamikaji

SOURCE:http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=4172
 
Back
Top Bottom