Mzee Mchopu
JF-Expert Member
- Sep 24, 2014
- 1,031
- 268
Wakuu ikiwa imebakia siku moja lile zoezi la bomoa bomoa liendelee kuna kesi ya kuomba kuzuia zoezi hilo mpaka kesi ya msingi kusililizwa.
Tafadhali kwa yoyote mwenye updates asisite kushea na jamii ya watanzania
Natanguliza shukrani.
============
Mbunge wa Kinonodon, Maulid Mtulya (katikati) akiwa sambamba na baadhi ya Mawakili wanaosimamia kesi ya kupinga kubomolewa kwa wakazi wa Mabondeni wa jimbo hilo la Kinondoni mapema leo Januari 4, muda mfupi baada ya kutoka kusikilizwa kwa kesi yao ya msingi ya kupinga kubomolewa.
Kesi hiyo ilifunguliwa na Mbunge huyo kwa kwa lengo la kutetea wananchi hao ili haki ipatikane na hatma ya wapi watapelekwa. (Picha zote na Andrew Chale).
Dar es Salaam
Umati wa wananchi wa Mabondeni ikiwemo bonde la Msimbazi, Magomeni Mkwajuni, Hananasifu, Magomeni Sunna, Kigogo na maeneo mengine wa Jimbo la Kinondoni wamefurika kwa wingi mapema kuanzia asubuhi ya leo katika Mahakama Kuu ya Ardhi iliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam kusikiliza kesi ya msingi ya kupinga kubomolewa nyumba zao iliyofunguliwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Mh. Maulidi Mtulia (CUF).
Mtulia amefungua kesi hiyo kupinga kubomolewa kwa wakazi hao bila kuwa na njia mbadala ikiwemo kupatiwa makazi mengine kwa wananchi wake yenye usalama zaidi.
Hata hivyoi Modewjiblog iliyokuwa katika eneo la tukio tokea asubuhi, ilishuhudia umati mkubwa wa wananchi wakifurika katika viunga vya Mahakama hiyo kiasi cha kufanya shughuli zingine za mahakama hiyo kusimama.
Baada ya masaa matatu, Jaji wa Mahakama hiyo Kuu ya Ardhi, Mh. Panterine Kente aliweza kusimamia kesi hiyo huku baadhi ya wananchi wakiwakilishwa na wajumbe zaidi ya saba, pamoja na wanasheria wa Mbunge huyo, ambapo maamuzi yalidumu kwa muda wa saa zaidi ya saa moja, na baadae Mawakili wa upande wa Mbunge wa Kinondoni, akiwemo Abubakari Salim aliweza kuutangazia wananchi hao pamoja na wanahabari kuwa, baada ya kupitia vielelezo vyote, kesi hiyo itatolewa hukumu kesho siku ya Jumanne, Januari 5.2016.
“Kwa shauri lililopo sasa linatarajiwa kutolewa jibu kesho Januari 5, Saa tano asubuhi ndio tutapata jibu kamili, kwa sasa tunarudi na tutakutana hapa hapa Mahakamani.” alieleza Wakili huyo.
Wananchi wanaopinga kubomolewa mabondeni wakiondoka katika eneo la Mahakama ya Kuu ya ardhi.
CHANZO: Mo Dewji
_____________________
UPDATE
BOMOA BOMOA YASIMAMISHWA KINONDONI NA MAHAKAMA KUUU (KITENGO CHA ARDHI)

Last edited: