Huku ni kuwatukana watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huku ni kuwatukana watanzania

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mtaka Haki, Oct 11, 2010.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  NINGEKUWA NA NAFASI YOYOTE YA UONGOZI CCM NINGEJIUZULU

  Nimekuwa nikiangalia kwa makini mwenendo mzima wa Kampeni za wagombea wa urais.

  Nimekuwa nikifuatilia masuala ambayo yangeitwa ni mazito kwa nchi.

  Nimengojea majibu ya masuala haya kutoka kwenye mdomo wa walioko serikalini na mgombea wa chama kinachotawala ili tu nipate sababu za kumpa kura.

  Kwangu mimi masuala mazito yamekuwa ni ufisadi mkubwa unaofanywa na watu waliokabidhiwa madaraka.
  Kwangu mimi viongozi wanaoiba raslimali za taifa na kujinufaisha basi inakuwa wazi kuwa sababu zao za kutafuta uongozi ni kuendelea kuiba.

  Nilidhani hii ni hoja nzito kuliko zote. Nilidhani nitasikia jinzi mianya ya rushwa itakavyozibwa. Jinsi wanaotumia vibaya madaraka watakakavyofanyiwa.

  Nilipata matumaini pale rais Jakaya Kikwete aliposimamia watu wakapelekwa mahakamani. Japo nilishangaa baadhi ya watuhumiwa wakubwa kama Mh Chenge ambao hata ushahidi wa wizi wao ulithibitishwa na wapelelezi wa kimataifa.

  Cha kushangaza mpaka leo sijasikia viongozi hawa waliokuwa madarakani wakisema chochote kuhusu hili. Badala yake Rais aliyeko madarakani bila woga wala shida yoyote amekwenda na kuwapigia debe hata wale aliokuwa amesema ndio ushahidi wake kuwa yuko makini kwa suala la rushwa.

  Hapa suala sio ufuai wa chama au chuki dhidi ya Kiongozi wetu mpendwa.

  Hapa ni suala la akili za kawaida na vipaumbele na vigezo tunavyotumia kusema kiongozi fulani anafaa na huyu hafai. Hapa sio sula la ushabiki wa chama. Hapa ni suala la ni nani atakayelinda raslimali za Tanzania?
  Ndugu zangu. Kama imefikia mahali watanzania tunaona ni sawa kuruhusu matusi haya yaendelee basi naomba mimi niwe simo.

  Hakuna njia nyingine ya kupeleka ujumbe kwa viongozi kuwa pamoja na kukupenda lakini hapa baba umekengeuka.

  Nilidhani pia kuwa rais hakutumia busara kukataa kura za wafanyakazi. Nilidhani kipindi hiki atakubali bila kumung'unya maneno kutamka kuwa nilikosea niwieni radhi naomba kura zenu na ni za muhimu. Kutokana na hayo naona hii ni kuwatukana watanzania na kuwaambia hamna akili kabisa.

  Kama watanzania hawatapeleka ujumbe wa kuonyesha kuwa wanahitaji uongozi makini kwa kuacha mbali ushabiki wetu wa vyama na urafiki katika mambo mazito basi ukweli ni kuwa Taifa la Tanzania tutakuwa tumelimaliza.

  Tutakuwa tunapeleka ujumbe kwa vizazi vijavyo kuwa kuiba sio shida. Cha muhimu ni uwe chama fulani. Kila utakachofanya basi ni sawa kama wewe ni wa chama hicho.

  Naisikitikia Tanzania iliyojulikana duniani kote kwa sababu ya uongozi madhubuti wa rais wa kwanza. Nasikitikia Tanzania ijayo itakayoanza kutokutoa uzito kwa mambo mazito.

  Bilioni moja ni pesa za kutosha kujenga shule za sekondari 10 kwa gharama ya milioni 100 kila shule. Mfano mdogo tu wa pesa za EPA shs Bilioni 133 zingejenga shule 1300. Hii ina maana pesa zingetumika kujenga shule zaidi ya 35 katika kila mkoa wa Tanzania.

  Haya ni mambo mazito. Tutazalisha mafisadi kama hatutakemea ufisadi bila kujali vyama au urafiki au undugu.

  Nilidhani Rais wangu mpendwa Mh Jakaya Kikwete atatumia nguvu nyingi kuonyesha msimamo mzito juu ya watu wanaojaribu kununua uongozi kwa fedha na kutaka uongozi kunufaisha biashara zao. Bado rais wetu hakufanya hivyo.

  Ungeniuliza ningemwambia baba hapa unatutukana kwani ungeonyesha heshima kidogo kwa hisia zetu juu ya uzito wa mambo tuliyodhani ni mazito. Hi ni kuidhalilisha taasisi ya urais.

  Ningekuwa niko kwenye chama cha mapinduzi leo na ningekuwa nagombea nafasi yeyote kwa heshima ya watanzania ningejiondoa na kujiuzulu angalao kusema kuwa sikubaliana na chama changu na inaoneka fikra za mwenyekiti kwenye haya ni ngumu.

  Kwa heshima ya watanzania na kwa heshima ya CCM wagombea na mliokuwa wanachama wa CCM jiondoeni kwa haki kuwa chama kimeshindwa kuonyesha kuwa kina umakini na raslimali na mali za watanzania ambao ndio uhai wetu.

  NAWAKILISHA
   
 2. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  mkuu hata paragraph hakuna? au ndo kuchoka kwenyewe?
   
Loading...