Habari za kazi,
Samahani kwa niaba ya wakazi wa Kimara, Kilungule ‘B’ naomba kuwasilisha kwenu hujuma ya huduma ya maji ambayo tumeipata kwa takribani miezi sita sasa.
Mtaa wetu umefanikiwa kupata miradi kadhaa ya uchimbaji wa visima vya maji kwa ufadhili wa wolrd bank, pia wapo wananchi kadhaa ambao nao wamechimba visima kwa lengo la kuuzia wananchi maji na wengi wa wananchi hao ni sehemu ya kamati ya maji ya mtaa na ndio chanzo cha hujuma ya maji ya serikali.
Kwa mda wa miezi sita sasa huduma ya maji ya serikali ya mtaa kupitia visima vilivyochimbwa na kukabidhiwa serikali ya mtaa imehujumiwa sana.
Sisi wananchi tumeishia kuteseka kwa kukosa huduma ya maji huku mwenyekiti akivunja kamati ya maji na kuunda kamati nyingine ambayo imeonekana kushindwa kabisa kutatua kezo za wananchi. Wananchi wamelipa madeni yao yote lakini kwa kipindi chote hiki cha miezi sita sababu zinazotolewa ni pamoja na Motor imeharibika, Pump imekufa, Umeme mdogo, Bomba limepasuka, na kila mara wananchi wamekuwa wakichanga michango lakini matatizo yamekuwa yakizidi kujitokeza.
Tunamashaka sana sana na utendaji wa serikali ya mtaa, Mwenyekiti wetu ( Bw Mchilla –0766 998892) sisi wananchi tunaomba ngazi ya juu waingilie kati, kero hii imekuwa kubwa sana na tunahisi hizi ni hujuma za wazi kabisa, tunaomba mkuu wa wilaya, uongozi wa DAWASCO, Wizara ya Maji na Mh Raisi wetu mpendwa ambaye kwa mda mfupi sana umekubalika na mamilioni ya wananchi.
Tunaomba mliangalie kwa jicho la tatu swala hili
Naomba Kuwasilisha