Hujuma: Kituo cha afya Makole (Makole health center)

Fiziolojia

JF-Expert Member
Oct 19, 2019
819
1,078
TUNAPOELEKEA NI KUBAYA.

..Kijana wangu jana usiku majira ya saa nne alimpeleka mgonjwa wake baada ya kuona amezidiwa katika kituo cha afya Makole kilichopo mjini kabisa katika jiji la Dodoma.

..Cha kushangaza, alipofika kituoni hapo kabla hajamshusha mgonjwa wake kutoka kwenye gari, mwanaume mmoja mtu wa makamo (inaonekana ndiye mlinzi aliyekuwa zamu), alikuja chap chap dirishani mwa gari na kumuambia kijana wangu kuwa huduma hakuna kwani kituo kimepuliziwa dawa, hivyo inabidi aende hospital ya mkoa ya dodoma (general hospital) akapate huduma za matibabu.

... Kusema kweli kijana wangu alishangazwa na kauli hiyo maana hali ya mgonjwa wake ilikuwa sio nzuri, na pia kwa utaratibu na mujibu wa muongozo wa wizara ya afya, matibabu yanapaswa kuanzia ngazi za chini, ili kama yatashindikana ndipo mgonjwa hupewa rufaa kwenda hospitali za ngazi ya juu (mfano, wilaya au mkoa).

Naomba ujumbe huu uwafikie wahusika ili hatua kali za kinidhamu zichukuliwe kwa huyo mlinzi, na pia uchunguzi ufanyike maana naamini kabisa huenda hiyo kauli ya mlinzi ni maneno aliyolishwa na watoa huduma kituoni hapo(siyo maneno yake).

.. Nasema hivyo kwa sababu mara kadhaa tu nimeshawahi kusikia kuwa nyakati hasa za usiku, na hasa wekend, watumishi wa makole walio zamu ya night (na hasa madaktari) wanaamua kutokutoa huduma kwa makusudi kabisa ili wakazurure mjini. Hivyo wanachokifanya kuchonga dili na mlinzi ili awaambie watu wanaokuja kupata huduma kituoni hapo waende general kwa sababu na visingizio kama mbalimbali.

..Na hata wale wagonjwa wanaowapokea, mfano wajawazito wenye uchungu ambao wangeweza kujifungua bila shida yoyote:(yaani bila ya operesheni), huwapa rufaa zisizo na tija kwenda general ama hospital nyingine ili wao aidha wapate mda wa kukala vizuri, au wakazurure mjini.

HII NI ZAIDI YA HUJUMA KWA WIZARA YA AFYA NA SERIKALI KWA UJUMLA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi hospitali za serikali ni vichekesho kweli saa nyingine kuna moja nilienda kuhudumiwa meno nakutana na mlinzi mlangoni ndiyo mtu wa kwanza kukukaribiaha hata salamu hamna lete risiti ukitoka uko ndan anakufungua na mdomo kuhakikisha kama hujang’oa ni hospitali ya mkoa wa kilimanjaro hata kama ni mapato sio kwa hatasimentnhizi kwa wagonjwa tunazofanyiwa na walinzi jmn

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TUNAPOELEKEA NI KUBAYA.

..Kijana wangu jana usiku majira ya saa nne alimpeleka mgonjwa wake baada ya kuona amezidiwa katika kituo cha afya Makole kilichopo mjini kabisa katika jiji la Dodoma.

..Cha kushangaza, alipofika kituoni hapo kabla hajamshusha mgonjwa wake kutoka kwenye gari, mwanaume mmoja mtu wa makamo (inaonekana ndiye mlinzi aliyekuwa zamu), alikuja chap chap dirishani mwa gari na kumuambia kijana wangu kuwa huduma hakuna kwani kituo kimepuliziwa dawa, hivyo inabidi aende hospital ya mkoa ya dodoma (general hospital) akapate huduma za matibabu.

... Kusema kweli kijana wangu alishangazwa na kauli hiyo maana hali ya mgonjwa wake ilikuwa sio nzuri, na pia kwa utaratibu na mujibu wa muongozo wa wizara ya afya, matibabu yanapaswa kuanzia ngazi za chini, ili kama yatashindikana ndipo mgonjwa hupewa rufaa kwenda hospitali za ngazi ya juu (mfano, wilaya au mkoa).

Naomba ujumbe huu uwafikie wahusika ili hatua kali za kinidhamu zichukuliwe kwa huyo mlinzi, na pia uchunguzi ufanyike maana naamini kabisa huenda hiyo kauli ya mlinzi ni maneno aliyolishwa na watoa huduma kituoni hapo(siyo maneno yake).

.. Nasema hivyo kwa sababu mara kadhaa tu nimeshawahi kusikia kuwa nyakati hasa za usiku, na hasa wekend, watumishi wa makole walio zamu ya night (na hasa madaktari) wanaamua kutokutoa huduma kwa makusudi kabisa ili wakazurure mjini. Hivyo wanachokifanya kuchonga dili na mlinzi ili awaambie watu wanaokuja kupata huduma kituoni hapo waende general kwa sababu na visingizio kama mbalimbali.

..Na hata wale wagonjwa wanaowapokea, mfano wajawazito wenye uchungu ambao wangeweza kujifungua bila shida yoyote:(yaani bila ya operesheni), huwapa rufaa zisizo na tija kwenda general ama hospital nyingine ili wao aidha wapate mda wa kukala vizuri, au wakazurure mjini.

HII NI ZAIDI YA HUJUMA KWA WIZARA YA AFYA NA SERIKALI KWA UJUMLA.

Sent using Jamii Forums mobile app

wasiliana na wasimamizi wa huduma Mganga Mkuu wa Kituo hicho namba 0783 336545 atakupa ushirikiano wako, kama huenda ulikereka kwa namna moja au nyingine ila kimsingi uchunguzi wa kilichotokea usiku ule na maada uliyoileta ni two different things kabisa hivyo tuwe wavumilivu wa kuangalia namna ya kutatua swala kwa kufuata taratibu na si kukimbilia mitandaoni.

Asante sana mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom