Hujamaliza kazi, upo duniani kwa sababu

mushijcob

Senior Member
May 20, 2015
104
69
Kila kitu kipo duniani kwa sababu. Wewe pia uko duniani kwasababu hauko duniani kwa bahati mbaya. Wewe kupumua leo ni sababu pia yapo mambo yanakupasa uyafanye. Je umeshatambua kwanini upo hai leo?

#Hujamalizakazi ndio hujamaliza kazi uliyotumwa kuifanya duniani. Na kama bado hujaitambua kazi mimi siweze kukuambia kazi yako rudi kwenye kile unachokiamini na kukisimamia utapata majibu sahihi rudi kwenye imani yako ya kiroho, nenda kule unapokulia kiroho.

Miili yetu haiwezi kufanya kazi bila roho zetu roho ndiyo inaongoza mwili ukiisahau roho utajikuta kila unachokifanya duniani hakina furaha kabisa.
Hujamaliza Kazi ya kubadili dunia.

Dunia ulivyoikuta unatakiwa uache mabadiliko usiondoke bila kuacha mabadiliko yeyote hapa duniani. Huko unapokwenda utadaiwa kwa kuchezea nafasi uliyopewa hapa duniani.

#Wako wengi wamekufa tena ni wema zaidi yako lakini wewe unapumua unafikiri ni bahati mbaya? Watoto wanazaliwa hospitali hawajafanikiwa hata kuona miti huku duniani wanafariki wewe upo hai bado unalalamika. Kua hai peke yake ni fursa kubwa sana.

Kuwepo siku ya leo ni fursa kubwa mno usichezee fursa hii ya uhai ulio nao. Nguvu ulizo nazo zitumie vyema kuleta mabadiliko katika ulimwengu huu. Ulimwengu unakusubiri wewe ufanye na utajitokeza kukusaidia anza leo fanya fanya fanya fanya fanya.

Usiogope kama unaandika andika hadi kila mtu ajue unaandika kama unaimba imba hadi kila mtu ajue unaimba maana siku ukifa hautapata tena nafasi ya kufanya chochote zaidi itakua ni majuto ukiwa peke yako ndani ya jeneza.

#Sasahivi unawaogopa watu unajua ukifa unaondoka mwenyewe unaowaogopa watabaki au watakufa kila mmoja kwa namna yake? Usiogope wala kutetemeshwa na chochote wote tutakufa na tutaicha dunia fanya kile moyo wako unakipenda na fanya kwa bidii hadi uache mabadiliko makubwa kwenye dunia hii.

#Kila mmoja angetambua kwamba anatakiwa aache alama duniani dunia ingekua ipo mahali pazuri sana kipindi hiki lakini hilo hatuwezi kulikulibadili tunachoweza kufanya ni yake ya kwetu yaliyotusababisha tuje hapa duniani.

#Hujachelewa bado haijalishi una miaka mingapi sasa kama upo hai na una ufahamu bado unaweza kufanya mabadiliko makubwa duniani. Hata kama upo kitandani huwezi kutembea unaweza kurecord sauti na maneno yako yakaacha mapinduzu makubwa hapa duniani.

Swali langu la mwisho kwako. #Unatumiajefursahii ya uhai ulionao leo?
 
Back
Top Bottom