Hufikiria vitu vya msingi nikiwa bafuni

Sep 10, 2019
72
74
Habari wadau
Muumba katuumba tofauti kimaumbile, kitabia, kisura na hata uwezo wa kufikiri.

Hali kadhalika kila mmoja huwa ana eneo lake mahususi (baa, chumbani, jikoni, sebuleni,chooni, bafuni,ofisini nk) ambalo hua anakua huru na linamfanya afikirie/ajipangie mikakati mbalimbali ya maisha yake.

Bafu ni chumba muhimu sana kwangu kwani ndiko ninakotumia muda mwingi kufikiria na kupanga mikakati ya maisha yangu, hua natumia dk 15-25 na hutegemea uzito wa wazo ninaloliwaza siku husika.

Binafsi nishaizoea hii hali na familia yangu ishanizoea xx kua nikiingia bafuni sitoki chini ya dk 15.

Je wewe huwaza vtu vya msingi ukiwa eneo gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata mimi bafuni ndo sehemu ya kupanga nyanga zangu kichwani ndo sehemu ninakua na utulivu wa hali ya juu.

The good, the bad and the ugly.
 
Back
Top Bottom