Huenda ni kweli mwandishi alikosea, lakini hii ndio 'polite language' ya kumjibu mtu mzima?

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,325
152,136
Mwandishi wa gazeti la Mtanzania aliwasiliana na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU,kamishina Mlowola kutaka kujua namna zoezi la kuwahoji wabunge wanaoutuhumiwa kutaka/kupokea rushwa katika hili sakata linaloendelea.

Sasa baada ya mwandishi kuwasiliana na kamishina huyo,majibu yalikuwa kama ifuatavyo;

"Leo ni lini?" alimuuliza kamishina Mlowola na mwandishi alimpomjibu kuwa ni Ijumaa,alisema: "Naomba tuheshimiane, niko kanisani kwa sasa."

Hivi ndivyo aya ya mwisho katika habari hii inavyosomeka na ndio aya ilioniacha hoi katika habari hii nzima.

Nini maoni yako hapa?

=========================

Mbunge aeleza alivyokwepa mtego wa rushwa

MMOJA wa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ambaye kamati yake imetuhumiwa kuhusika na rushwa, ameeleza jinsi alivyotaka kupewa fedha zinazodaiwa kuwa za rushwa na moja ya idara za Serikali, lakini akazishtukia na kuzikataa.

Mbunge huyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini, amesema wakiwa katika moja ya vikao vya kamati aliitwa na kiongozi wake na kuambiwa wameitiwa ‘lunch’ (chakula cha mchana), lakini si kwa maana ya kupatiwa chakula, bali fedha.

“Nilikuwa kwenye majukumu yangu, nilipoambiwa kuna ‘lunch’, yaani fedha kutoka kwenye moja ya idara tulizokuwa tunazikagua, niliwasiliana na Katibu wa kamati yetu kumuuliza kama jambo hilo lipo sawa sawa na akanishauri kwamba nisishiriki,” alisema Mbunge huyo.

Siku tatu baada ya kuibuka kwa kashfa ya rushwa miongoni mwa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) tayari imewaita kuwahoji wabunge waliokuwa wanaunda kamati tano zilizofanyiwa mabadiliko na Spika Job Ndugai.

Zaidi ya wabunge saba tayari wameitwa na kuhojiwa na Takukuru, wakiwamo wale waliotajwa kuhusika kuomba rushwa na ambao hawajatajwa.

Baadhi ya wabunge walioitwa kuhojiwa Takukuru juzi licha ya kuwasilisha barua ya kujiuzulu kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai baada ya kusikia tuhuma hizo ni pamoja na Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT- Wazalendo), Zitto Kabwe na wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe.

Taarifa za kuwepo kwa rushwa zimeibuka hivi karibuni, huku Spika wa Bunge, Ndugai, akifanya mabadiliko ya baadhi ya wajumbe wa kamati na kuwaondoa baadhi ya wenyeviti wa kamati hizo.

Katika mabadiliko hayo yaliyowagusa wabunge 27 na kamati tano za Bunge, Spika Ndugai ametoa maelekezo ya kujazwa kwa nafasi zao zilizoachwa wazi na wenyeviti na makamu wenyeviti mara moja.

Hata hivyo, akizungumza hivi karibuni, Ndugai alisema mabadiliko hayo hayana uhusiano na tuhuma za rushwa.

“Tumefanya mabadiliko ya kamati kwa lengo la kuboresha tu utendaji, ni kama kocha una timu yako unataka kukiimarisha tu kikosi, wala siyo tuhuma za rushwa,” alisema Ndugai.

Kwa upande wake Zitto, alithibitisha kupata wito kutoka makao makuu ya Takukuru ili kuhojiwa juu ya sakata hilo na akapongeza kuwa endapo vyombo vya Serikali vitakuwa makini kushughulikia tuhuma zote zinazoelekezwa kwa wanasiasa na watumishi wengine wa umma, itasaidia kuongeza uwajibikaji na kupunguza uzushi kwa wananchi.

“Nimepata wito huo kupitia Ofisi ya Bunge. Nasikia Bashe ameitwa pia. Nafurahi wito wetu wa uchunguzi umechukuliwa kwa uzito unaostahili na tutatoa ushirikiano wote kwa vyombo vya uchunguzi ili kumaliza zoezi hili kwa haraka na kwa ufanisi,” alisema Zitto.

Alipoulizwa na gazeti hili sababu ya kukimbilia kujiuzulu mapema, Zitto alijibu kupitia mtandao wa Whatsapp kuwa uamuzi huo ulilenga kuvishinikiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi ili kubaini ukweli.

“Kujiuzulu kwangu ni kushinikiza uchunguzi. Ni namna tu ya kutaka jambo hilo lipewe uzito unaostahili…Kwa uelewa wangu, najua hakuna lolote. Nilikuwa kwenye kamati siku nzima sikuona linalozungumzwa.

“Kama kuna watu walikuwa na mchezo, hilo silijui. Muhimu kwangu ni kwa kamati yetu kuchunguzwa na kama kuna waliofanya kinachofanywa wachukuliwe hatua,” alisema Zitto.

Hadi kufikia Machi 24, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ilikuwa imeshawahoji wabunge zaidi ya saba.

Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu zoezi hilo, Mkurugenzi wa Takukuru, Kamishna Valentino Mlowola, alikataa kuzungumzia mwendelezo wake, akisema yuko kanisani.

“Leo ni lini?” aliuliza Kamishna Mlowola na mwandishi alipomjibu kuwa ni Ijumaa, alisema: “Naomba tuheshimiane, nipo kanisani kwa sasa.”

Chanzo: Mtanzania
 
Yani mnawafata watu mpaka makanisani tena Ijumaa Kuu awa waandishi wa magazeti ya Chadema wanatafuta choko choko ili wapate matukio ya kuuza magazeti yao.
Hili jibu ni wazi boss huyu wa TAKUKURU amejenga mtazamo hasi ama na mwandishi au gazeti husika.

Hivi angekuwa ni mwandishi wa HabariLeo au wa gazeti la Uhuru haya ndio yangekuwa majibu?
 
Mate sitemi alikuwa na uharaka gani wa kumpigia simu siku ya Ijumaa Kuu.?
kiongozi wa serikali anapaswa kutkuwa na ijumaa kuu wala jumapili lakini kwa serikali hii ya maigizo ndio tuna watu kama akina mlowola anajifaanya Mungu badala ya kumpa muda siku yeye anasahau kwamba uongozi ni dhamana na cheo ni dhamana na yupo pale kwa ajili ya kodi za wananchi
 
Mwandishi wa gazeti la Mtanzania aliwasiliana na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU,kamishina Mlowola kutaka kujua namna zoezi la kuwahoji wabunge wanaoutuhumiwa kutaka/kupokea rushwa katika hili sakata linaloendelea.

Sasa baada ya mwandishi kuwasiliana na kamishina huyo,majibu yalikuwa kama ifuatavyo;

"Leo ni lini?" alimuuliza kamishina Mlowola na mwandishi alimpomjibu kuwa ni Ijumaa,alisema: "Naomba tuheshimiane, niko kanisani kwa sasa."

Hivi ndivyo aya ya mwisho katika habari hii inavyosomeka na ndio aya ilioniacha hoi katika habari hii nzima.

Kwa taarifa zaidi tembelea: www.mtanzania.co.tz

Nini maoni yako hapa?
Tatizo la waandishi wengi wa nchini hspa ni kuwa wengi ni ma F4F na hawijishughulishi kufanya utafiti kabla ya kusaka habari.
Sasa kwa mtu aliye kanisani au msikitini , utafiti mdogo tu wajinsi ya kutafuta habari hugeuza zoezi zima kuwa ni la kuudhi.
 
Angemjibu "nipo kanisani nipigie baadaye",labda anamuiga JPM alivyokuwa anawajibu vibaya waandishi wa habari siku alipowaapisha mawaziri.
 
Tatizo la waandishi wengi wa nchini hspa ni kuwa wengi ni ma F4F na hawijishughulishi kufanya utafiti kabla ya kusaka habari.
Sasa kwa mtu aliye kanisani au msikitini , utafiti mdogo tu wajinsi ya kutafuta habari hugeuza zoezi zima kuwa ni la kuudhi.
Kiongozi makini anapaswa kuwa "humble".

Kiongozi anapaswa kuwa muangalifu anapohojiwa au kuongea na waandishi wa habari.Sometimes mwandishi anaweza,tena kwa makusudi, kukuuliza swali la maudhi na wewe ukahamaki ukajibu vibaya na yeye akapata story ya kukuandika au hata kuonyesha ni jinsi gani usivyokuwa na busara kama kiongozi.
 
Kama mwansishi anajua ni zoezi linaloendelea angetumia common sense tu kwamba siku ya kazi atauliza maswali yake. Alitengeneza emergency isiyokuwepo.
 
Kiongozi makini anapaswa kuwa "humble".

Kiongozi anapaswa kuwa muangalifu anapohojiwa au kuongea na waandishi wa habari.Sometimes mwandishi anaweza,tena kwa makusudi, kukuuliza swali la maudhi na wewe ukahamaki ukajibu vibaya na yeye akapata story ya kukuandika au hata kuonyesha ni jinsi gani usivyokuwa na busara kama kiongozi.
Mtu makini zaidi ata conclude kuwa mwandishi ana upungufu wa akili, kumuumbua mtu si story endelevu.
 
Back
Top Bottom