Huduma za wajawazito zimebadilika

Huduma za wajawazito zimebadilika

lubano jr

Member
Joined
Apr 25, 2019
Posts
67
Reaction score
118
Utaratibu wa mjamzito kuanza kliniki zimekua na changamoto kubwa kwa hasa wananchi wa kipato cha chini. Nimehudhuria kliniki kwa mara ya kwanza nikiwa na mke wangu kama taratibu zao zinavyosema kwenye hospitali ya serikali ya Tandale lakini utaratibu wanasema umebadilika.

Kuanza kupata huduma ni lazima ulipie kuanzia kadi ya kumuona daktari Tsh 2000/= akuandikie vipimo vyote zaidi ya 6 ambayo gharama yake ni Tsh 15,000/= ndio mjamzito aanze kliniki, kama huna uende nyumbani.

Sasa nimejiuliza kwa hawa wenzangu na mimi wasiokuwa na kipato watahudumiwa na nani? Serikali iliangalie hili kupitia Wizara ya Afya watoto wengi watazaliwa majumbani tena wakiwa na matatizo kibao ambapo serikali itakuja kutumia nyingi kununua chanjo na madawa.
 
Shida sio kulipia Ila nawaonea huruma hao wenye kipato cha chini, ndio shida.
 
Sasa hiyo ni pesa gani ya kuja kulalalmika hapa...??? Matibabu ni ghali ila vipimo ni ghali zaidi
 
Kuwa na aibu basi... hivi hiyo ni hela ya kulia lia mtandaoni? Kama hiyo ni nyingi sasa watoto mnaleaje? Msituchoshe na nyuzi za ajabu ajabu
 
Back
Top Bottom