Dah,kiukweli wananchi tunateseka sana.ukitaka kuona ninalolisema nenda kituo cha kimara kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa moja,watu wanasukumana hovyo kama unaumwa unaweza anguka na kukanyagwa.
ndo maana nikashauri kama ni kweli kuna upungufu wa magari,waruhusu wamiliki wa dala dala waanzishe route za mbezi kariakoo na posta ili kusaidia wananchi wakati huyo mwekezaji anajipanga.