Hubert Velud ni kocha mpya wa Simba Sports Club kutoka Ufaransa

ndio ataikuta tayari playlist ya wachezaji ya wazee wa simba mezani,huyu tunamtaka huyu hatumtaki na hapo hapo watu wanataka matokeo ya haraka,huyo hata hatakaa,atarudi ufaransa na malapa tuu
 
Sioni ajabu mkuu kutimuliwa. Timu yenye kuweza kukaa na kocha muda mrefu ni Arsenal pekee duniani, angalia Zidane juzi katoka kuwapa mataji lakini tetesi zimeanza.
Jirekebisheni wana msimbazi..ujio wa Mo uwaweke sawa
 
Tatizo la simba sio kocha bali ni mfumo mbovu katika uendeshaji timu. Kwa mfano kuna baadhi ya wachezaji UNTOUCHABLE/GODFATHER ndani ya timu
 
Hivi kuna kundi maalumu la makocha wa kizungu limetengwa kwa ajili ya afrika tuu. Maana naona kila timu zikileta kocha mzungu takuta anazururura kufundisha vi timu vya afrika tuu
 
Mmh hapo sidhani kama Simba walijiridhisha vyema kwa maana nijuavyo atakuja na mfumo wake tofauti na huu, sasa hapo kwenye ubadilishaji mfumo timu ikiboronga tu kidogo huyo hana chake
Simba wanahisi wana wachezaji bora kuliko timu yoyote ya Ligi Kuu, na kwa hivyo hawapaswi kuhangaishwa na timu yoyote ya Ligi Kuu au kwengineko Tanzania hii na hata Afrika ya Mashariki yote. Wanaamini kwamba kutoridhisha kwa kiwango cha timu yao kunasababishwa na makocha walio nao, wakisahau kwamba walijiridhisha (kama walivyojiridhisha kwa huyu Mzungu) awali kabla ya kuwateua. Uhalisia ni kwamba Simba wana mchanganyiko wa wachezaji aina nne: 1. Wachezaji hodari lakini wanaoshindana zaidi na umri kuliko wachezaji wenzao uwanjani. 2. Wachezaji vijana wenye uwezo lakini bado hawajakomaa 3. Wachezaji vijana wenye uwezo mkubwa lakini waliokata tamaa kwa sababu moja au nyengine 4. Wachezaji vijana wenye uwezo mkubwa lakini wanaolemazwa na kudekezwa mpaka wakajiona wakubwa kuliko timu. Sidhani kama kuna atayemfunulia kocha huyo mpya ukweli huu. Na bila ya ukweli huu, Simba itabaki kuuguza majeruhi ya Okwi na Niyonzima huku kina Mlipili wakisubiri Nyoni aumie. Hata watapoamua, mathalan, Ndemla aingie uwanjani akiwa bado na msongo wa mawazo ya safari ya Sweden, bado kina Kichuya wataendelea kucheza na mfundo moyoni kwa sababu hakuingizwa mchezaji waliyemtarajia wao. Wataendelea hivyo mpaka Haji Manara atapopata wasaa mwengine wa kuwabembeleza. Unategemea kocha atamudu vipi kuonesha uwezo wake kwenye mazingira ya aina hiyo?
 
huyo kocha hajui kama timu haina uwanja wa mazoezi
kwa bongo hata aje kocha wa viwando vya UEFA hakuna kitu, tatizo ni
-aina ya wachezaji, hawafundishiki kwa level ya juu,hawana misingi ya soka
- viongozi wa vilabu ni mambumbu wa soka management
- hakuna miundo mbinu ya kusapoti soka la kisasa,viwanja vya mazoezi nk
- mpaka aina ya wananacha na mashabiki wengi ni oya oya tu. simba ndani ya miaka mitatu imebadili makocha wengi mnooo, mwenye idadi atusaidie, ina maana wotee hao hawajui ? . wananchama na mashabiki oya oya utawasikia wakisema eti kikosi kikubwa kuliko mwalimu,hivi simba kuna mchezaji gani mkubwa wa kiwango hata kucheza wydad ambae anaukubwa kuliko omog aliefundisha vilub vikubwa kuliko simba. lazima tubadilike, haya njoo ila utajuta kuijua bongo soka utakapoanza kupangiwa usajiri .
 
kwa bongo hata aje kocha wa viwando vya UEFA hakuna kitu, tatizo ni
-aina ya wachezaji, hawafundishiki kwa level ya juu,hawana misingi ya soka
- viongozi wa vilabu ni mambumbu wa soka management
- hakuna miundo mbinu ya kusapoti soka la kisasa,viwanja vya mazoezi nk
- mpaka aina ya wananacha na mashabiki wengi ni oya oya tu. simba ndani ya miaka mitatu imebadili makocha wengi mnooo, mwenye idadi atusaidie, ina maana wotee hao hawajui ? .

Umeanza vizuri uchambuzi wako kuwa kuna tatizo kwa wachezaji wa Tanzania kupokea mafundisho sahihi ya kocha.

Lakini maneno yako ya mwisho hapo hayana mshiko, kubadilisha kocha hata ulaya wanafanya hivyo pamoja na changamoto zote lakini timu lazima iwe na malengo, hivi unajua Manchester United toka ajiuzulu Alex Ferguson wamepita wangapi? Je wote walikuwa hawajui?
 
Simba wanahisi wana wachezaji bora kuliko timu yoyote ya Ligi Kuu, na kwa hivyo hawapaswi kuhangaishwa na timu yoyote ya Ligi Kuu au kwengineko Tanzania hii na hata Afrika ya Mashariki yote. Wanaamini kwamba kutoridhisha kwa kiwango cha timu yao kunasababishwa na makocha walio nao, wakisahau kwamba walijiridhisha (kama walivyojiridhisha kwa huyu Mzungu) awali kabla ya kuwateua. Uhalisia ni kwamba Simba wana mchanganyiko wa wachezaji aina nne: 1. Wachezaji hodari lakini wanaoshindana zaidi na umri kuliko wachezaji wenzao uwanjani. 2. Wachezaji vijana wenye uwezo lakini bado hawajakomaa 3. Wachezaji vijana wenye uwezo mkubwa lakini waliokata tamaa kwa sababu moja au nyengine 4. Wachezaji vijana wenye uwezo mkubwa lakini wanaolemazwa na kudekezwa mpaka wakajiona wakubwa kuliko timu. Sidhani kama kuna atayemfunulia kocha huyo mpya ukweli huu. Na bila ya ukweli huu, Simba itabaki kuuguza majeruhi ya Okwi na Niyonzima huku kina Mlipili wakisubiri Nyoni aumie. Hata watapoamua, mathalan, Ndemla aingie uwanjani akiwa bado na msongo wa mawazo ya safari ya Sweden, bado kina Kichuya wataendelea kucheza na mfundo moyoni kwa sababu hakuingizwa mchezaji waliyemtarajia wao. Wataendelea hivyo mpaka Haji Manara atapopata wasaa mwengine wa kuwabembeleza. Unategemea kocha atamudu vipi kuonesha uwezo wake kwenye mazingira ya aina hiyo?
Hapo kocha hawezi kudhihirisha uwezo wake kwa aina hii ya wachezaji waliopo msimbazi..we subiri miezi michache ijayo wataanza kumsaka mchawi nani
 
Mkuu hivi kule Jangwani mlipofanya Hans Pluijm- Lwandamina, lengo lenu lililokuwa nini? Na hasa ukizingatia alipata mafanikio. Tuanzie hapo kwanza
 
punguza povu kwanza mkuu twende sawa
Nimekuliza kwa kunukuu kama ulivyosema, masuala ya miezi michache ijayo wataanza kumsaka mchawi umesema wewe mkuu. Sasa povu liko wapi?

Jibu mkuu nilivyokuuliza mkuu
 
kuna siri ndio lakini nyie hamchelewi mnajulikan tu..muda utasema
 
Back
Top Bottom