UBORA
+ Simu hiyo ni US$ 150.00 tu
+ Inatumia Windows Phone 8 OS
+ Ina Apps Maalum kwa Afrika
UDHAIFU
- Ina HD yenye ukubwa wa 4GB (Ingawa uwepo wa memory card slot utasaidia)
Kampuni ya Huawei ikishirikiana na Microsoft wamefanya uzinduzi rasmi wa simu inayojulikana kama Huawei 4Afrika, maalum kwa soko la bara la Afrika. Hatua hii inaonyehsa wazi kwamba kampuni kubwa zinaanza kuliona bara la Afrika kama soko muhimu kwa ajili ya kuwekeza. Uzinduzi wa simu hii ni sehemu ya juhudi za Microsoft kuwekeza katika teknolojia Barani Afrika, mradi huo wa Microsoft unajulikana kama 4Afrika.
Simu hiyo iliyozinduliwa siku chache zilizopita inatumia Windows Phone 8 na pia inakuja na apps ambazo zinaendena na hali ya soko hilo na kwa mujibu wa Microsoft zimetengenezwa na Waafrika. Kwa mujibu wa GSM Association Africa ni bara la pili kwa kutumia simu nyingi za mobile baada ya Asia na pia ndio soko linalokuwa kwa kasi kubwa zaidi kuliko masoko yote katika simu za mkononi.
SOURCE NA MAKALA HII KWA UKAMILIFU:
Gajetek - Gajet na Teknolojia: Microsoft na Huawei wazindua Simu ya Afrika