Housegirl: Ushauri


Good advice Von Mo
 
(Natamani ningepewa mi hio kazi ya kuwasakizia watu)...

Mi kweli hazi ya kusakizia siiwezi, natamani nikupe wewe hiyo kazi ila kama we ni HE, mmmmhhh, naogopa usijefanya mapinduzi bure
 

My boy sio mapepe hata kidogo, I raised him so namjua vizuri. Naweza kusema kuwa na yule mdada ilikuwa bahati mbaya tu na isitoshe dogo alipagawishwa na yule mama sukari (si unajua mimama sukari hupenda watoto wadogo)
 

Asante kwa ushauri wako
 

Nakubaliana na wewe kuwa kumtaftia kijana mchumba/mke kunaweza sababisha lawama ila hilo la housegirl kutokubadilika na kuwa na mwazo ya maendeleo nakataa, hii ni tabia ya mtu tu, mbona Joyce Kiria alikuwa house girl?
 
Unachokipenda wewe siyo atakachokipenda mwengine....
Siri kubwa ya ndoa ni kuwa inatoka kwa MUNGU na wala sio kwa matakwa au matamanio ya mtu fulani...
Yes House maid ni mzuri kitabia na muonekano but yet that aint a credit...
Kinachokusumbua ni kuwa umeshampenda huyo binti na ukasahau kuwa ni moyo wako ndio uliomfagilia na si wa mwanao...
 
mwenzangu wacha kijana achague mwenyewe usitake lawama, yalishanikuta nilimpa mke mtoto wa mama yangu mkubwa
anavyo mfanyamkewe utadhani mtumwa na akimwambia kwanini anasema kwani mie ndio nimekutaka si hao mashawishi ndio
wameniletea kituko wewe,hapa najuuuuta lakini ndio wameshaa zaa watoto 4...
 

kakuruhusu nani kumchagulia mwanao mchumba wa kuoa? Huoni kuwa unamkosea kwa njia moja ama nyingine? Nafikiri wewe kaa kushoto, ana akili timamu, ana mapenzi yake, ana mapigo yake. Pia two years inakupa uhakika gani kwamba huyo HG wako ni mzuri wa kuolewa na mwanao?

Kuna vitu vingine huna authority ya kufanya hivyo. Mwache ikifika siku ataoa tu kwa kuchagua mwenyewe.
 

Wadada wa kisasa mnamomonyoa maadili ya kiafrika mwache atafute kitu roho inapenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…