fourtypercent unachosema ni kweli, kumtafutia mtoto kazi ya u-house boy/girl inaweza kuwa si jambo zuri endapo watoto hao wataangukia kwenye mikono ya akina baba/mama wapenda dogodogo au akina baba/mama wasiojali utu na heshima ya watoto wa wenzao. Wapo baadhi ya watu walionufaika na kazi hizo kwa kusomeshwa na kutafutiwa maisha na mabosi wao.
Ila pia wapo walioambuliwa kubakwa, kunyanyaswa, kutukanwa na kudhalilishwa na baadhi ya mabosi wao. Kikubwa nafikiri si aina ya kazi, bali kuwe na mabadiliko ya kitabia kwa wazazi wanaoajiri ma-house girl/boy na kulinda heshima na utu wao. Ni vyema kuwatreat watoto/ndugu hawa kama watoto/ndg zetu wa karibu. Tuache ukatili maana hata sisi tusingepata elimu na vijikazi vya hapa na pale, huenda tungeangukia huko hususan kwa nyakati hizi ambapo ajira imekuwa ni tatizo ...
Nafikiria pia kipuuzi, tusingekuwa na mahouse girl/boy, hali za familia zetu kwa sisi tunaoishi mijini ingekuwaje? Naomba nisinukuliwe hapa wala kueleweka vinginevyo, ni fikra tu .....