GE2025 Hotuba za Wanasiasa kwenye nyumba za Ibada zinadumisha amani na maadili ya Uchaguzi, au zinapotosha wapiga Kura na kuathiri uadilifu wa mchakato?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Tanzania inakaribia Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025. Joto la siasa limekuwa likipanda na kushuka, na majukwaa yanazidi kutafutwa, ikiwemo Nyumba za Ibada. Lakini je, hii ni sawa?

Wanasiasa wanapohutubia kwenye Makanisa au Misikitini, wengine husema wanajenga maadili, amani na mshikamano. Lakini Je, Siasa kwenye nyumba za Ibada ni sehemu ya ustaarabu wa demokrasia au ni uvunjaji wa mipaka ya heshima ya imani? 🕌⛪🗳️

Wanaweza kusema ''tunaomba dua'' au ''tunashukuru kwa neema ya uongozi,'' lakini ujumbe wao mara kadhaa hugeuka kuwa kampeni ya kisiasa kwa maneno. Je, wapiga kura hawaathiriki Kiimani au Kifikra?

Tunapoelekea Oktoba 2025, ni muhimu kujiuliza, Siasa ndani ya nyumba za Ibada zinadumisha amani na maadili ya uchaguzi, au zinapotosha mwelekeo wa wapiga kura?
 
Waraka wa TEC ndo mpango
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…