LIKUYU SEKA
Member
- Nov 15, 2013
- 53
- 24
·- HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KATIKA IBADA YA MAADHIMISHO YA JUBILEE YA MIAKA 125 YA INJILI YA KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI MBUYUKENDA, TANGA TAREHE 05 JULAI, 2015
Mheshimiwa Baba Askofu, Dkt. Stephen Munga, Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki;
Waheshimiwa Maaskofu;
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Magalula Said Magalula;
Waheshimiwa Wageni Wote Toka Ndani na Nje ya Tanzania;
Waheshimiwa Wana-Dayosisi na Wananchi Wote Mliopo Hapa;
Mabibi na Mabwana;
Bwana Yesu Asifiwe:
Nakushukuru sana Baba Askofu Stephen Munga kwa kunialika na kunishirikisha kwenye ibada hii ya kihistoria ya Maadhimisho ya Miaka 125 ya Injili katika Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. Kwa kweli ni jambo la furaha na heshima kubwa kwangu kujumuika na Maaskofu na waumini wa Kanisa hili kwa tukio hili kubwa na la kihistoria.
Mwaliko wenu huu kwangu ni uthibitisho wa uhusiano mzuri uliopo baina ya KKKT na Serikali nchini. Uhusiano ambao umekuwa na manufaa makubwa kwa nchi yetu na watu wake. Uhusiano ambao umejitafsiri katika umoja, upendo, amani, na mshikamano uliopo baina ya Watanzania wa rangi zote, dini zote, makabila yote na wa popote watokako na walipo.
Maadhimisho ya Miaka 125
Mheshimiwa Baba Askofu,
Waumini Wote na Wageni Waalikwa;
Siku kama ya leo, miaka 125 iliyopita ndio siku ambayo Wamisionari wa Kijerumani wa Bethel wapoliwasili mahala hapa. Kwa maelezo yako, walipachagua hapa kuwa ni mahala pa kuwahifadhi vijana waliokombolewa kutoka utumwani. Hivyo mahala hapa paliwapa uhuru, na matumaini mapya watu ambao walikwishakata tamaa. Aidha, kutokea hapa, ndipo kazi ya injili ilipoenea na kusambaa mkoani Tanga. Kusimama na wanyonge, kuwafuta machozi na kuwatua mzigo wao, ni jambo la heri, ni jambo jema na ni jambo linalompendeza Mungu. Na huo ndiyo msingi imara wa Kanisa hili.
Huo pia ndiyo msingi ambao juu yake imejengeka kazi na wajibu wa Serikali. Sisi katika Serikali tunao wajibu wa kuwaondolea wananchi unyonge, kuwapunguzi umaskini, kuwalinda na kuwakinga dhidi ya dhuluma na uonevu na kuwajengea msingi bora wa maendeleo yao. Jitihada zetu za kuondoa umasikini, kutoa fursa za elimu, kuboresha huduma za afya na mambo mengi mengineyo tufanyayo yana malengo hayo.
Jitihada za Serikali zinapounganika na zile za madhehebu ya dini tunatengeza nguvu kubwa ya kuwaondolea wananchi wetu siyo tu unyonge wa kiroho, bali pia kuwapunguzia changamoto za maendeleo zinazowakabili na kusaidia kuinua hali zao za maisha.
Mchango wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki
Waheshimiwa Maaskofu, Ndugu Wananchi;
Ninaposema hivyo, natambua mchango wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki katika kuwaletea maendeleo jamii na watu wa Mkoa wa Tanga. Mimi ni shahidi, maana nilifika kule Magamba, Lushoto mwaka jana kufungua ukumbi wa kisasa katika Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa (SEKOMU) kilichojengwa na Dayosisi hii. Pamoja na Chuo Kikuu, natambua mnazo shule za sekondari za Lwandai, Bangala na Dinari.
Dayosisi hii inatoa pia huduma za kipekee ambazo hazipatikani kwa urahisi hapa nchini. Ninyi mna shule ya wasioona ya Irente, shule ya msingi ya watoto wenye ulemavu wa ubongo (Autism) na kituo cha kutunza wagonjwa wa akili cha Lutindi.
Kwa upande wa Afya nako mmefanya mambo makubwa. Tunawashukuru kwa hospitali teule ya Wilaya ya Kilindi (Kilindi CDH) ambayo nilishiriki kuweka jiwe la msingi na kuizindua. Aidha nawapongeza kwa Hospitali yenu ya Bumbuli kuwa Hospitali Teule ya Halmashauri ya Bumbuli. Hatua hiyo itaimarisha pia Chuo cha Waganga Wasaidizi (Clinical Officers Taining College) cha Bumbuli.
Napenda pia kupitia sherehe hii kuwashukuru ninyi wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania kwa kazi yenu nzuri muifanyayo. Vile vile, nawashukuru sana kwa kuiunga mkono Serikali katika jitihada za kuwaletea maendeleo Watanzania. Nawaomba muendelee na moyo huo mwema. Namuomba Mwenyezi Mungu awaongezee pale mlipopunguza na kuendelea kuwashushia baraka tele.
Mheshimiwa Baba Askofu,
Serikali inatambua na kuthamini sana ushirikiano baina yake na madhehebu na mashirika ya dini. Ndiyo maana tumekuwa tunatengeneza mazingira mazuri kwa mashirika ya dini kuendesha shughuli zake. Tumekuwa tunatoa msamaha wa kodi, tunatoa mikopo kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu vyenu na kutoa ruzuku kwa ajili ya uendeshaji wa zahanati, vituo cha afya na hospitali ambazo Serikali inaingia ubia na Kanisa katika kutoa huduma kwa wananchi.