tikatika
JF-Expert Member
- May 6, 2011
- 2,330
- 4,119
Hapa ni sehem ya kujifunza mambo mbali mbali. Kimsing nimejifunza vingi sana kupitia JF. Kwa hiyo ninapo leta mada nategemea mawazo mapya toka kwa mtu mwingine.
Sasa kupitia hotuba mbali mbali za viongozi wetu na hata wa nje ya nchi tumejifunza na tumeona hotuba nyingi sana, kimsing hotuba zote huandaliwa na kusomwa . Lakn namna ya usomaji ndio hutofautiana. Kuna usomaji wa kuwakilisha ujumbe wa mtu tutaita umesoma hotuba kwa niaba ya; Lakn kuna kuhutubia mkutano hii hutokea pale mtoa hotuba huivaa hotuba na husoma kwa ujanja sana. Sana sana akipitia vichwa vya paragraph ili kuwafanya wasikilizaji wake wakamwona anaongea nao.
Ndugu wana jf hebu tufuatilie hotuba mbali mbali hata mashulen mhusika akiwa ameiva na kile anachokitoa kiukweli anashawishi kumsikiliza.
Nampongeza mkapa alikua anajua kuhutubia hotuba ndefu lakn haichoshi kuisikiliza na kumtizama maana unajihisi anasema na ww. Na hata jk alikua anajiandaa na hivyo kutoa kile alichokiaandaa.
Lakn mkuu wetu kule AU alikua kama katumwa kumuwakilisha mtu mwingine na hotuba sio yake. Alishindwa kumeza baadhi ya maneno ili awe anatizamana na wasikilizaji wake.
Namwaminia sana kwa kumeza vitu, maana ana kumbukumbu ila kwa ile hotuba ameonyesha alikua na hofu kusimama mbele ya wenzie. Maana muda wote alikuwa amekodolea karatasi tu, na hainuki kuwatizama anaowahutubia.
OMBI
Watu wa protokali huyu ni rais wetu wote tafadhali mpeni semina namna ya kutoa hotuba itakayoonyesha yeye ndiye mwenyenayo. Kumbukeni popote anaposimama rais wa Tanzania tunasimama sisi. Zingatia kwa uzito wa uzinduzi wa jengo lile Tanzania ndio iliyokua inatizamwa na wajumbe wote na huku wakijiuliza je kiongozi wa huko amevaa viatu vya Nyerere japo hata kidogo? Wanaambulia kusomewa hotuba kama katumwa!! Mwalimu alikua akianza kuzungumza watu wote huwa kimyaaaa!! Sasa rais wetu anasoma ndio kwaaaanZa wenzio wanabadilishana mawazo!! Daa kiukweli imenisikitisha sana.
. Kumbuka mimi siongelei katumia lugha gani hata kama kingekua kisukuma ila ningependa kuona mzungumzaji avae anacho kizungumza.
Watanzania tuna mengi sana ya kujifunza ndani ya miaka hii mitano