Hotuba ya Joseph Mbilinyi yakatishwa baada ya kukaidi maagizo ya kuondoa kurasa zenye utata

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Hotuba ya Waziri kivuli wa Habari Joseph Mbilinyi yakatishwa baada ya kukaidi maagizo ya kutoa baadhi ya kurasa zenye utata katika hotuba hiyo bungeni.

Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu ameagiza Hotuba ya Kambi ya Upinzani kuhusu Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ihaririwe na kufuta maneno yote katika kurasa 17.

Zungu ametoa uamuzi huo leo asubuhi baada ya kipindi cha maswali na majibu, hata kabla ya bajeti yenyewe kuwakilishwa na Waziri Dk Harrison Mwakyembe.

Zungu amesema amezipihitia hotuba zote na kubaini kuwa ile ya upinzani itakayowalishwa na Joseph Mbilinyi 'Sugu' ina masuala yaliyopo mahakamani ambayo yamekwishazuliwa katika bajeti zilizotangulia.

Amesema maneno yenye mwelekeo huo yakisomwa atachukua hatua.

C_Db9BwWAAA95ph.jpg
 
  • Thanks
Reactions: SDG
maccm sijui wanahisi kuzuia hizo hotuba ndio kutapunguza matatizo ya wananchi!
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Nilimsoma Zitto sehemu noja akisema kuwa iliwachukua wabunge wengi wa ccm kuelewa kuwa tumepigwa kwenye rada, huenda ikawachukua miaka kumi pia kuelewa anachomaanisha Sugu na kujua kuwa ni wao wenye faida nacho hata kuzidi aliyekiwakilisha!
 
maccm majinga sana sasa sijui wanahisi kuzuia hizo hotuba ndio kutapunguza matatizo ya wananchi!
Kwani hata huyo Sugu akizisoma hizo hotuba za matusi ndio zitapunguza matatizo ya wananchi? We ovyo kabisa!
 
Hizi kurasa zenye utata huwa ni za upande mmoja tu au!! Napita tu nitarudi akishaziondoa.
 
Back
Top Bottom