Hotuba ya JK mwisho wa mwezi julai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya JK mwisho wa mwezi julai

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by De chris, Aug 8, 2012.

 1. D

  De chris Member

  #1
  Aug 8, 2012
  Joined: Aug 1, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivikaribuni Rais wa jumuhuri ya muungano wa Tanzania alilihutubia taifa kwa staili yake kwa kupitia waandishi wa habari. Tunampongeza sana rais wetu kwa utaratibuwake huo aliojiwekea.pamoja na mambo mengine aliyoyazungumzia pia aligusia mgomo wa walimu uliolimbima nchi mzama.Tunampongeza sana JK kwa kutambua mchango wa walimu katika kulijenga taifa letu. Pamoja nakuonesha msimamo wa serikali ,madai ya walimu ya sipuuziwe hata kidogo.Tumeshuhudia miaka michache iliyopita kulitokea mgomo wa walimu kama huu na serikali kama ilivyo ada ikadai kuwa mgomo huo haukuwa halali. Likini madhara ya mgomo ule yanaonekana hadi leo,tija katika ufundishaji imekuwa ndogo, matokeo yake wanafunzi elfu tano waliochanguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka jana hawajui kusoma wala kuandika.Serikali imekuwa ni sehemu ya watu wanaoshangaa eti haijui sababu nini.Kilio cha walimu kimekuwa cha muda mrefu.kumbuka walimu hutumia muda wao mwingi kufanya kazi za mwajili wao wawapo kituoni hata nyumbani kwa kufanya maandalizi kwaajili ya kufundishi siku ya inayofuata na kusahihisha kazi za wanafunzi. Walimu hawana kipato cha ziada kama ilivyo kwenye kada zingine.Mh.rais na serikali yake wajaribu kuangalia jinsi gani ya kutatua matatizo ya walimu yaliopo ili kuboresha maslahi ya walimu. Kwakufanya hivyo itaongeza motisha kwa walimu na kuboresha elimu kwa ujumla. Ni vema pia madai ya walimu yakawekwa bayana na umma usipotoshwe ,ni ukweli usio pingika kwamba madai ya walimu sio mishahara midogo tu bali hata mazingira yakufundishia sio mazuri,zana duni za kufundishia posho ya kufundishia,posho yakufanya kazi kwenye mazingira magumu,ukosefu wa nyumba za kuishi n.k Hivi ni kweli serikali imshindwa kutatua matatizo hayo hata kwa awamu.Serikali isibweteke kufumbia macho mambo muhimu kama hayo kukimbilia mahakamani sio “solution”kama kweli elimu ni kipaumbele basi lazimaserikali iwekeze kikamilifu,ipunguze matumizi yasiyo ya lazima na kuwekeza kwenye huduma za jamii ikiwemo elimu.poleni sana walimu kwa kukosa kibarua cha sensa hiyo ni hali halisi ya serikali za kibantu zilivyo azipendi kuambiwa ukweli.
   
Loading...