Hotuba aliyotoa Zitto Kahama tarehe 7/1/2017 na kuitwa ni uchochezi hii hapa

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
620
1,543
------------
Hotuba aliyotoa Zitto Kahama tarehe 7/1/2017 na kuitwa ni uchochezi hii hapa

Nimalizie kwa jambo la mwisho kubwa sana la kitafa lakini si kubwa sana

Leo hii sisi tupo hapa tunaongea na ninyi kwa sababu kuna uchaguzi mdogo Mwaka Jana mwezi Wa Sita Mkubwa mmoja alikuja na amri ya kuzuia mikutano ya hadhara mpaka 2020 hakuna mikutano ya hadharavyama vya siasa vimeundwa na katiba na sheria na inaturuhusu kufanya mikutano

Tusipofanya mikutano ninyi mtajuaje kama chama tawala kinavurunda,? Ndiyo maana ya mfumo Wa vyama vingi lakini bwana Mkubwa yule akazuia mikutano na baadhi ya watu wakamuunga mkono.

Lakini mungu nae ana yake kuna kampeni je atazuia mikutano ya kampeni? Mungu amemuonyesha kuwa kuna Mkubwa zaidi yake licha ya yeye kuwa Mkubwa katika nchi yake

Lakini wananchi kwanini haki hii ya kiraia zikanyagwe,Rais anapata wapi uwezo huu Wa kusema hakuna kufanya siasa wapi anapata halafu viongozi wengine wanamuangalia

Haki ya kufanya mikutano ni haki yetu ya kikatiba haipaswi tusubiri chaguzi ndogo ndiyo tuje kuzungumza na ninyi.

Lazima tuje kuwaambia mambo yanapokuwa hayapo sawa leo vyakula vimepanda bei ukame unakuja kuna baa la njaa tunasema kwa kuwa kuna uchaguzi Mdogo,kama hakuna mambo haya tusingeyasema eti kwa kuwa bwana Mkubwa mmoja kaamua.

Leo hii kuna wabunge wamewekwa ndani miezi na dhamana haitoki kila siku mbunge anapelekwa mahakamani na kurudishwa tu hakuna dhamana

Huyu mtu amechaguliwa na watu wake wananchi zaidi ya laki tatu lakini huyu mtu mmoja kwa kuwa ana jeshi,Magereza usalama Wa Taifa mizinga na risasi mahakama unamchukua kiongozi huyu kutoka Magereza unampeleka mahakamani na kumrudisha mahabusu kisa unamkomoa

Leo inawezekana tukaliona hili ni sawa kwa sababu kafanyiwa mtu Wa chama kingine kafanyiwa Lema ni Wa Chadema eti haituhusu!

Ninawaambia.wakifanikiwa kwa Lema watafika kwa kila mmoja wetu na wote tutawekwa ndani kama hatukemei mambo haya lakini haya yanafanyika hata viongozi wastaafu nao hawastuki wamekaa kimya

Ndugu zangu wana Isagehe juzi Rais alikuwa Bukoba ambapo watu wameharibikiwa Nyumba zao wamepoteza ndugu zao na mbaya zaidi wananchi mbali mbali wakawasidia lakini Rais badala ya kuwafarriji anawaambia kila mmoja atabeba mzigo wake haya si maneno ya kiongozi Wa serikali kuwaambia watu wake

Niwakumbushe tulikuwa na mtu anaitwa Cleopa Msuya katika bajeti ya kwanza ya Rais Mwinyi Msuya akiwa.Waziri Wa.fedha akazungumza bungeni kuwa halo ngumu kila mmoja aubebe mzigo wake huyu aliondolewa ofisini baada ya Siku tatu

Mnamkumbuka Mramba aliposema watanzania watakula majani ilimradi ndege inunuliwe leo yupo wapi?

Leo Rais anaenda Bukoba anawaambia kuwa ni watu Wa majanga tu kwamba tetemeko.lao ukimwi wao kunyauka migomba no wao na kisha anawaambia wataubeba mzigo wao hii si kauli ya kiongozi.

Sisi watanzania tumeumbwa na viongozi wetu wameumbwa kuwa wanyenyekevu,ndiyo maana ninashaangaa Mwinyi yupo wapi?,Mzee Mkapa yupo wapi Kikwete yuko wapi kwanini wako kimya

Viongozi wastaafu wako wapi kumuonya huyu Rais Magufuli ambaye anashindwa kuwa mnyenyekevu mbele ya wananchi waliompa kura huyu anakula Burr,anavaa bure analala bure kwa kodi zetu sasa madaraka yamempanda kichwani
 
Uchochezi umekuwa kitu cha kawaida sana kwenye utawala Wa awamu ya Tano........

Najiuliza roho aliyonayo kiongozi wetu angekuwa yeye ndiye mkoloni kipindi kile mwaka 1961..........

Nyerere angepotezwa na wala hasingeweza kuleta Uhuru miaka hiyo.....

Tungekuwa na historia tofauti kama ambavyo tumeingia kwenye historia tofauti............
 
Mtanange huu ni kwa hisani ya Msoga,enzi za Dau lauvuvi wa mafao na Mkwere toka kwetu Pwani Zitto alikuwa hakamatwi wala kusukwasukwa,kazi yake ilikuwa kuibusu kazi ya wadau na kuidukua CHADEMA ielekee kibra mbele ya CCM!!

Maisha yanaenda kasi ila ni fundisho pia kwa wazalendo wanafiki!!
 
Na kodi halipi huku akiwa mkali kwa mtu mwingine asipolipa kodi
 
Team Lowassa mungu alitupa maono lakini tukapuuzwa. Nashindwa kuwapa pole na pole yangu naipeleka kwa Team Lowasa na wazazi wangu.Magufuli atatawala hadi miaka kumi hilo linajulikana. Tafakari kama utamudu kuishi katika kifungo cha nje kwa muda huo wote la sivyo iga tu maisha ya kuzamia hata kama hupendi.
 
Ivi kwan ni lazima kila kitu kikisemwa ambacho wewe hukipendi lazima kiitwe "uchochezi"?
 
Back
Top Bottom