Masista (nuns) wawili toka Tanzania walialikwa kwenda kutembelea Marekani. Walikuwa wamesikia mengi juu ya "fast foods" za Marekani na jinsi Wamarekani wengi wanavyozipenda. Basi siku moja wakiwa matembezini wakakuta banda la chakula wakasogelea ili nao wapate kujipatia chochote. Mazungumzo yakawa kama ifuatavyo;
Sister 1: Excuse me sir, what are those things called?
Muuzaji: These are hot dogs sisters, would you like some?
Sister 2: Do people eat dogs here in USA? We don't eat dogs in our country
Muuzaji: Hey we don't eat dogs here, we eat hot dogs, that is a different thing altogether. Hot dogs is the most popular fast food in the US, everyone here eats hot dogs, including Obama!
Wale masister wakasemezana wao kwa wao;
Sister 1: Mwenzangu, sielewi anachosema. Labda na sie tujaribu iwe siri yetu. Ila sister usije ukamwambia mtu
Sister2: Hamna tabu sister, kwanza mie kwetu tuna asili ya kula nyama ya mbwa.
Basi wale masister wakamwambia muuzaji awape hot dogs mbili, na wakaondoka huku wakila.
Sister 1: Mmh, hivi mwenzangu umepewa sehemu gani ya mbwa kwenye mkate wako?
Sister 2: Yaani Sister naona aibu kuitaja, ila ni tamu ajabu! Watanzania wakigundua utamu wake watamaliza mbwa wote mitaani!