Hospitali za umma lango la kuzimu

Hospitali za umma lango la kuzimu

Ghost Worker

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2016
Posts
1,412
Reaction score
1,868
Tunashukuru sana kwa serikali ya awamu ya tatu kwa kuanza kufuatilia ubora wa elimu inayotolewa na taasisi zetu za elimu katika harakati za kuitafuta Tanzania tunayoitaka.

Japo hatua zimeshachukuliwa kwa baadhi ya vyuo vinavyotoa elimu ya tiba vilivyokuwa vinatoa elimu chini ya viwango vinavyohitajika, tunaiomna serikali iunde tume maalum kufuatilia hata wale watumishi wa sekta ya afya ambao walihitimu vyuo hivi na wengineo wote waliopo mahospitalini (hasa za umma) wachunguzwe kama wana sifa za kuendelea kutibu binadamu.

Wengi wa hawa wataalamu kutoka vyuo hivi ndio wanatutibu sisi masikini tusio na mahali pa kusemea wala uwezo wa Kwenda India na South Africa. Hali ni mbaya SANA SANA kwenye hospitali za umma. Uzembe, maadili mabovu na Rushwa kwa wataalamu wetu wa afya vinatuua jamani. Malalamiko ni mengi mno sijui tuyapeleke wapi!

Hospitali za umma si vituo vya tiba tena ni vituo vya kuongeza maradhi na wakala wa mtoa roho. Kwa mfano nimekuwa likizo nyumbani Mbinga kwa mwezi mzima, sasa hivi hospitali ya Wilaya ukipata tatizo linalolazimu upasuaji basi ndugu wanaanza kuandaa matanga. Tumeshazika wawili katika kadhia na mazingira ya namna hii (ninaowafahamu), sasa sijui kwa nchi nzima hali ikoje.

Mimi si mtaalamu wa haya mambo ya afya, kwa hiyo siwezi kuuzungumzia tatizo lilivyo kiundani zaidi. Jambo la msingi serikali itafute namna ya kuwasikiliza raia wake katika hili ili itambue ukubwa wa tatizo na kulifanyia kazi hali si nzuri hata kidogo.
 
Ndugu pole kwa yaliyokukuta na nakuomba uwamini madaktari wenu maana huwa wapo makini mno na hawapendi mgonjwa afe. Lakini pia maslahi duni kwa madaktari inasababisha madaktari wanakosa motisha na kutokujituma sana kumuangalia mgonjwa kila wakati. Fikiria mtu anafanya kazi sehemu mbili kilasiku kwa hiyo inamfanya achoke na kupitiwa kidogo kufuatilia mgonjwa. Kingine pia VIFAA duni husababisha wagonjwa kufa maana hakuna ICU YA UKWELI. Kingine pia UCHACHE WA MADAKTARI BINGWA, serikali inatakiwa iwajili mabingwa kila wilaya kushughulikia kesi ngumu. Lingine pia ndugu ni uwepo wa maabara Duni. Yaani daktari anaorder kipimo kikubwa mfano CT scan,CCP , na unakuta ni emergency na hakuna kwa hiyo humfanya daktari kuwa kama daktari wa kienyeji.PIA LINGINE ukosefu wa dawa. Dawa unakuta zipo lakini za aina moja na chache. Sasa insmuweka daktari kuwa na wakati mgumu sana kutoa matibabu.
 
Tunashukuru sana kwa serikali ya awamu ya tatu kwa kuanza kufuatilia ubora wa elimu inayotolewa na taasisi zetu za elimu katika harakati za kuitafuta Tanzania tunayoitaka.

Japo hatua zimeshachukuliwa kwa baadhi ya vyuo vinavyotoa elimu ya tiba vilivyokuwa vinatoa elimu chini ya viwango vinavyohitajika, tunaiomna serikali iunde tume maalum kufuatilia hata wale watumishi wa sekta ya afya ambao walihitimu vyuo hivi na wengineo wote waliopo mahospitalini (hasa za umma) wachunguzwe kama wana sifa za kuendelea kutibu binadamu.

Wengi wa hawa wataalamu kutoka vyuo hivi ndio wanatutibu sisi masikini tusio na mahali pa kusemea wala uwezo wa Kwenda India na South Africa. Hali ni mbaya SANA SANA kwenye hospitali za umma. Uzembe, maadili mabovu na Rushwa kwa wataalamu wetu wa afya vinatuua jamani. Malalamiko ni mengi mno sijui tuyapeleke wapi!

Hospitali za umma si vituo vya tiba tena ni vituo vya kuongeza maradhi na wakala wa mtoa roho. Kwa mfano nimekuwa likizo nyumbani Mbinga kwa mwezi mzima, sasa hivi hospitali ya Wilaya ukipata tatizo linalolazimu upasuaji basi ndugu wanaanza kuandaa matanga. Tumeshazika wawili katika kadhia na mazingira ya namna hii (ninaowafahamu), sasa sijui kwa nchi nzima hali ikoje.

Mimi si mtaalamu wa haya mambo ya afya, kwa hiyo siwezi kuuzungumzia tatizo lilivyo kiundani zaidi. Jambo la msingi serikali itafute namna ya kuwasikiliza raia wake katika hili ili itambue ukubwa wa tatizo na kulifanyia kazi hali si nzuri hata kidogo.
Nina kubali kuna wataalamu wa afya ambao hawana sifa, lakini siwezi sema wengi kwa sababu sina uwezo wa kutoa statistics.
Mara nyingi sana huwa tunalaumu wataalamu hawa bila kujali wanaokoa maisha ya watu wangapi. Kama unataka kujua wanaokoa maisha ya watu wangapi funga hospitali unayoona haitoi huduma nzuri uone kama kutatokea tofauti.
Unaweza ukafiwa na wandugu wawili au watatu, lakini kuna watu wengine hamsini wamepona.
 
Pole mkuu,upo sehemu gani huko?..Maguu,Matiri,Kipololo,Litembo au hapo mjimwema,jimboni,tangi la maji au msimbazi?.Likizo njema kwako
 
Madaktari wetu hawa balaa tupu, nikiwa mdogo magoti yalijaa maji, tulipokwenda Hosp ya wilaya walinipiga x ray wakashauri nikatwe mguu, Mimi nilikataa maana goti halikuwa linauma pamoja na kuvimba. Tukaenda mhimbili daktari akasema nna allergy nikapewa dawa nikapona. Ningemsikiliza daktari wa kwanza nisingekuwa na mguu hii Leo.
 
Njoo hapa Hospitali ya MAFINGA ujionee!

Kuna shetani mtoa roho kama Daktari Mkuu wa Hospitali hii.
 
Ila madaktari wengine kwakweli mmmh wakaguliwe tu vyeti vyao..... Watatuua
Vyeti sio ishu Ndugu. Unaweza ukawa na mabanda ya Afya lakini unakosa rasilimali kutibu kitaalamu na kuwa sawa na mganga kienyeji. Serikali ijatahidi iongeze mishahara kwa madaktari maradufu na pia iboreshe vifaa vya tiba na uchunguzi. Mabingwa wasambazwe kila wilaya ili kesi ngumu wazimanage na bila kusahau wapewe vifaa tiba. KWA Hiyo serikali ijitahidi kuzarisha mabingwa na wao wapewe ukuhu wa idara na sikupeana cheo kwa experience. Fikiria unakuta mkuu wa idara wa TB ni CO na sio MD au bingwa. Yaani wilayani huko kufanya kazi kwa mazoea inafanya huduma inakuwa mbovu.
 
Back
Top Bottom