Hospitali ya Serikali, Zakhem Mbagala imulikwe.

Kyenju

JF-Expert Member
Jun 16, 2012
4,558
1,500
Hii kadhia imeipata moja ya familia ambayo niko karibu nayo. Kisa chenyewe kilikuwa hivi, Mama mmoja katika familia hiyo alipatwa na matatizo yaliyosababisha ujauzito kutoka. Alipo kwenda Hospiali Daktari akamwambia anatakiwa kusafishwa, akamtaka atoe 100,000 hiyo pesa alichukua Daktari (Rushwa), akasafishwa na kurudi nyumbani. Baada ya siku kadhaa yule mama hali yake ikawa mbaya na ngozi ya mwili ikaanza kubadilika, akarudi pale Hospitalini akamkuta Daktari mwengine tofauti na yule wa mwanzo. Baada ya kumcheck akamwambia kuwa alisafishwa vibaya hivyo inakiwa asafishwe upya tena kwa kufanyiwa Operation, akaambiwa atoe 180,000 (rushwa). Kwa kuwa hawakuwa na pesa ya kutosha ikabidi jamaa zake waende kuileta hiyo pesa wajati huyu mama akiendelea kufanyiwa operation. Kibaya zaidi kuna mama mjamzito alikuwa anasubiria kuingia chumba cha upasuaji kujifungua kwa njia ya Upastaji aliachwa kwa maana hakuwa na pesa ya kuhonga. Baadaye yule mjamzito alipofanyiwa upastaji, mtoto alikutwa amefariki.
 

kwamtoro

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
4,929
2,000
Mishahara ya madaktari ni midogo, wanaogopa kuandamana. Wanayapenda sana meno yao na macho yao.
 

124 Ali

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
7,671
2,000
Kutoa taarifa sehemu husika pia inahusu(takukuru) la sivyo mpango utaendelea hivyo hivyo kila siku.
 

Mkempia

JF-Expert Member
Mar 5, 2013
1,142
1,500
Hizi hospitali za serikali kwa kweli zinahitaji kuangaliwa kwa jicho la tatu! Nimeshakutana na kituko cha hospitali ya serikali hivyo naelewa muanzisha thread anachoeleza.
 

Kyenju

JF-Expert Member
Jun 16, 2012
4,558
1,500
Hizi hospitali za serikali kwa kweli zinahitaji kuangaliwa kwa jicho la tatu! Nimeshakutana na kituko cha hospitali ya serikali hivyo naelewa muanzisha thread anachoeleza.

Tatizo hawa jamaa wanaendekeza njaa.
 

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
31,338
2,000
Hospitali za serikali kwa rushwa, ni majanga kuanzia wahudumu, manesi hadi madaktari
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom