Hospitali ya Mwendakulima, Kahama lugha chafu kwa wahudumu zimezidi ichunguzeni

MfalmewaKiha

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
1,191
1,231
Habari zenu wadau,

Niende kwenye Mada husika,
Kiukweli katika jamii hospitali ni sehemu nyeti sana kwani mtu anapo hisi Afya kuzorota NDIO sehem peke ya kukimbilia,

Cha Ajabu hii hospitali ya MWENDAKULIMA_KAHAMA,ni tofauti na kile wengi wanacho kitegemea,

1_Wahidumu wa pale huwezi fanikiwa kumpata mhudumu mwenye lugha ya upendo, ukarimu nk, wote ni kama wanahasira hasira, Ukimsemesha semesha unaweza kupewa Tusi ambalo hujategemea.

2_. Hospitali Nzima haina dawa, cha Ajabu dawa unapoandikiwa unaelekezwa kwenda kununua kwa moja ya manesi (Nyumbani)hapo hapo jirani na hospitali,
Mbaya zaidi sio dukani,dawa zipo ndani kwao wanako ishi,

3_ 79% Ya Manesi wanavaa Nguo fupi ambazo ziko juu ya magoti. Sasa akinama kidogo kwakweli watu Wanapatwa na Mfadhaiko w Moyo

4_ Usafi wa humo ndani ni mdogo sana, Hospitali inanuka yani haina mfano

5_. Wauguzi hawana Haraka ya kumhudumia mgonjwa,Yani ukifika pale inaweza kuchukua dakika 45 ndo upewe huduma

6_ Wamama Wajawazito kati ya 10 Basi 4 hupoteza maisha,

NB: Kwa atakae bisha juu ya haya nitakuja na video,

Tunaiomba serikali yetu iwaangalie upya maana imefikia hatua mpaka wananchi wanaiogop hiyo Hospitali hivyo kuwalazimu kwenda umbali fulani kutafuta huduma za afya

Naomba kuwakilisha.
Matusi sitaki
 
Kama Kweli Kati Ya Kumi 4 Wanapoteza Maisha Basi Hiyo Hospitali Ingeshafungwa, Ila Mimi Nakupongeza Sana Kwa Kutoa Taarifa Ila Pia Ukitoa Taarifa Muhimu Kama Hii Usiongeze Mbwembwe Kuipa Uzito Unaiharibu, Mfano Unapozungumza Habari Za Nguo Na Vingine.

TUTALIFANYIA KAZI
 
Kama Kweli Kati Ya Kumi 4 Wanapoteza Maisha Basi Hiyo Hospitali Ingeshafungwa, Ila Mimi Nakupongeza Sana Kwa Kutoa Taarifa Ila Pia Ukitoa Taarifa Muhimu Kama Hii Usiongeze Mbwembwe Kuipa Uzito Unaiharibu, Mfano Unapozungumza Habari Za Nguo Na Vingine.

TUTALIFANYIA KAZI
Wewe ni mhusika?
 
Wewe mama acha wivu.

Tutakulipua na wewe usipotulia.Uliachishwa kazi serikalini kwa sababu ya vyeti feki na umeajiriwa sehemu nyeti.Leo unatuletea majungu eti manesi wanavaa nguo fupi!Unataka wavae madera hospitalini?

Suala la kuwepo kwa dawa unataka watumishi ndio wanunue kwa pesa zao?
 
Naisikia tuu hiyo hospitali,sitamani hata kwenda maana jina lenyewe tuu{joke}linantishaa,..hata KWEMA naona wanaanza tabia hii sijui ni stress au malipo duni,.dah!!!
 
Hiyo hoja no. 3 imetia dosari taarifa yako. Kwa mtazamo wangu kuvaa nguo fupi ni miongoni mwa mbinu za kutoa huduma bora kwa wateja. Kama hayo mengine yana mapungufu yarekebishwe
 
Mkuu nikiwa kama Kada na mshabiki mkubwa wa Chama cha Wananchi nashauri uambatanishe ushahidi wako wa ukweli ili hili swala likome hapo kwenye vifo vya wajawazito ni idadi ya kutisha kwa uwiano huo tafadhali leta ushahidi tuone ili kesho tu nifike hapo nimalize tatizo ambatanisha hizo video plzzz
 
Mi napenda hospital ya manesi wanaovaa nguo fupi napenda sana kuona mapaja hii inasababisha nikachek afya Mara kwa mara hata kama siumwi..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom