Hospitali ya Muhimbili Kuanza Kupandikiza Figo Mei 2017

Hashpower7113

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
1,353
2,140
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) imesema itaanza kutoa huduma ya kupandikiza figo kuanzia Mei, 2017. Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Tiba wa Hospitali ya Muhimbili, Dk. Hedwiga Swai amesema kwamba kwa kipindi kirefu, serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kuwasafirisha wagonjwa kwenda nje ya nchi, jambo ambalo limewafanya wajipange kuanza kutoa huduma hiyo hapa nchini.
Dk. Swai amesema kuwa hospitali hiyo ipo kwenye hatua za mwisho wa urekebishaji wa vyumba vya upasuaji. Kuanza kufanyika kwa upasuaji wa kupandikiza figo nchini, sambamba na kuboreshwa kwa huduma ya kuchuja damu kwa watu wenye matatizo ya figo (dialysis) kutawasaidia mamilioni ya Watanzania wanaoteseka lakini hawana uwezo wa kwenda nchini India, pia kutaokoa mamilioni ya fedha ambazo serikali na watu binafsi wamekuwa wakitumia kufuata matibabu nchini India.
Hayo yatakuwa ni mapinduzi makubwa katika sekta ya afya nchini, tangu serikali ilipofanikisha kuanzishwa kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, ambapo sasa wagonjwa wa moyo kutoka nchini na nchi nyingine za Kiafrika, wanatibiwa Muhimbili, tena kwa ufanisi mkubwa.

Tazama video....YouTube
 
Back
Top Bottom