Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kinara wa kutoa mimba kwa wanawake na wanafunzi!

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,685
22,694
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaonya Madaktari vinara wa Hospitali ya Rufaa ya Songea ambao wanasifika kwakufanya biashara ya kutoa mimba wanawake na wanafunzi kuacha tabia mara moja,lasivyo atawafukuza kazi na kuwafunga jela.

Waziri Mkuu alitoa onyo hilo jana wakati alipotembelea Hospitali hiyo na kuzungumza na watumishi kwa lengo la kuwasisitiza kutoa huduma bora kwa wagonjwa,ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 3mkoani Ruvuma.

Alisema Hospitali ya mkoa huo inasifika kwa kutoa mimba wanawake na kuwalazawagonjwa wao wodi namba 5, kitendo ambacho serikali haikuruhusu wala haikubaliani nacho."Naomba mkuu wa mkoa fanya ziara ya kushtukiza katika wodi namba 5 utakuta wanawake wametolewa mimba, wakiwemo wanafunzi na kisha madaktati hao wanatumia wodi zetu kuwalaza wagonjwa wao waliowatoa mimba.Ni marufuku na nitawachukulia hatua kwani majina ya madaktari hao ninayo," alisisitiza majaliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa alimuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa huo,Dr. Daniel Malekela na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dr. Phils Nyimbi kuwafuatilia madaktari wanaojihusisha na vitendo hivyo na kutoa taarifa ili wachukuliwe hatua kali.

Pia, alimuagiza mganga mkuu Dkt Daniel Malekela kuondoa duka lake lililo jirani na hospitali hiyo ili kuondo hisia kwamba dawa zinaibiwa na kupelekwa kwenye maduka ya watumishi.

Chanzo: AFRICAN MAGAZINE
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1452139379022.JPG
    uploadfromtaptalk1452139379022.JPG
    16 KB · Views: 27
Last edited by a moderator:
Huyo Mganga Mkuu Daniel Malekela elimu haijamsaidia ni bure kabisa. Ameweka duka lake la dawa hapo nje ya hospitali halafu kaandika maandishi makubwa kwenye bango MALEKELA PHARMACY .....I mean seriously !!!!!!!
 
Huyo Mganga Mkuu Daniel Malekela elimu haijamsaidia ni bure kabisa. Ameweka duka lake la dawa hapo nje ya hospitali halafu kaandika maandishi makubwa kwenye bango MALEKELA PHARMACY .....I mean seriously !!!!!!!

Sasa angeliweka wapi???? Hapo si ndio kuna wateja???

Heri ya mwaka mpya.
 
Sasa angeliweka wapi???? Hapo si ndio kuna wateja???

Heri ya mwaka mpya.
Hilo Swali ungemuuliza Mh. Waziri Mkuu na kwa nini amepewa amri ya kuliondoa hapo mara moja.
Dr Mwaka hajambo!? Heri ya mwaka 2016 na Kwako pia.
 
Back
Top Bottom