Hospitali ya Bugando haina TC Scan, X-Ray | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hospitali ya Bugando haina TC Scan, X-Ray

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bitabo, Dec 17, 2011.

 1. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2011
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  HOSPITALI ya Rufaa ya Bugando (BMC) ambayo imeadhimisha miaka 40 toka kuanzishwa kwake inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uharibufu wa mara kwa mara wa mashine za TC-Scan pamoja na X-ray na kusababisha ugumu wa utoaji wa huduma kwa wagonjwa.

  Uharibifu wa mashine hiyo tangu Septemba 2010 umesababisha kusitishwa kwa huduma hiyo ambapo wagonjwa wanaotakiwa kufanyiwa kipimo hicho cha TC–Scan hulazimika kusafirishwa hadi katika hospitali za Muhimbili au KCMC iliyopo mkoani Kilimanjaro.

  Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari, mkurugenzi wa hospitali hiyo, Charels Majinge alisema kuwa pamoja na kukusanya Sh200 milioni kwa mwezi kama mapato ya hospitali hiyo, bado wameshindwa kutengeneza mashine hizo kwa wakati kutokana na gharama kubwa zinazohitajika.

  Hata hivyo alisema kuwa kati ya mashine mbili za CT-Scan walizonazo wanatarajia kutengeneza moja mara tu kifaa cha UPS ambacho kinauwezo wa kupima wingi wa umeme kufungwa katika haspitali hiyo.

  “Matatizo ya kukatika kwa umeme mara kwa mara na ndiyo chanzo cha kuungua kwa mashine hizo ambayo kila moja inagharimu Sh4 billion fedha ambazo ni nyingi sana ”alisema dk Majinge.

  Aidha hospitali hiyo inakabiliwa pia changamoto za ununuzi wa madawa ambayo yanaandikwa na madaktari bingwa ambayo hayapatikani katika bohari ya madawa ya MSD.

  Akitoa ufafanuzi wa upatikanaji wa madawa Dk Majige alisema kuwa BMC inapata vifaa vya asilimia 20 hadi 40 kutoka MSD na kusema kuwa asilimia hiyo ni ndogo sana kwa kuzingatia dawa nyingi ambazo ni muhimu na gharama za juu hazipatikani katika bohari hiyo. Alisema kuwa changamoto zote hizo zinahitaji uwezo mkubwa wa kifedha katika kuyatatua na kuwa pingamizi kubwa katika malengo yao ya kutoa huduma bora ya afya na tiba kwa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo.

  Pamoja na hayo, uongozi wa hospitali hiyo umejipanga kutafuta fedha kutoka kwa wafadhili mbalimbali wakiwemo watu wenye makampuni makubwa, taasisi nawatu binafsi.

  Alisema hospitali hiyo ina matarajio mengi ikiwemo mpango wa kuendeleza na kuimarisha utafiti wa tiba kwa kuanzisha taasisi ya utafiti wa tiba ili kutimizwa malengo ya tatu ya kuanzishwa kwa hospitali hiyo.

  source: mwananchi ya leo

  ETI TUNASEMA TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE. What a hell !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...