Hospitali nzuri ya kwa mjamzito

Temporary01

JF-Expert Member
May 12, 2011
260
70
Habari za kazi wadau?

Mkewangu ni mjamzito, ndio mimba ya kwanza na ina takriban wiki ya nne sasahivi.
Naomba ushauri wa hosipitali nzuri itakayo mfaa ukizingatia yeye ana changamoto kadhaa za kiafya zinazo mkabili.
Changamoto zenyewe ni kuwa, mosi yeye ana tatizo la moyo la muda mrefu aliambiwa tatizo lake hali hitaji upasuaji hivyo atumie dawa na litakuja kuisha lenyewe. Ametumia dawa kwa miaka kadhaa na Namshukuru Mwenyezi Mungu sasahivi hali yake ni nzuri kiasi kwani ana muda mrefu haja tumia dawa na hajapata tatiozo.

Pili yuko under weight kwa muda mrefu, naweza kusema ndio mwili wake tangu nime mjua mpaka nime muoa. Tatu, alifanyiwa operation mwaka jana mwezi wa kumi, alikuwa na uvimbi kwenye mirija ya uzazi na ulichelewa kugundulika mpaka ukapasukia ndani, Namshukuru sana Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma kwa kumuokoa manake sijui ningekuwa na hali gani wakati huu.

Nne, takriban mimba mbili zilisha toka zikiwa katika wiki za mwanzo kabla hata ya kufika mwezi, na amekuwa akisumbuliwa na magonjwa mara kwa mara has UTI na MALERIA.

Kwenye suala la Hosipitali, Uzuri nao maanisha ni huduma zao, gharama na uwezo wa hosiptali husika kushuhulikia mgonjwa iwapo zitajitokeza complications zozote kama upasuaji nk. Pia hosipitali inayo tumia bima za NHIF ndio hasa nazo zipendelea kwasababu bima anayo, hivyo nahitaji hosiptali yenye kugharamia matibabu yote kwa kutumia bima, ikiwa ni kuchangia basi kiwe kiasi kidogo tu.

Kwa kumalizia, sisi tupo Dar es Salaam, hivyo naomba ushauri kwa hosipitali za Dar.

NB: Kwa wale wenye uzoefu au hata wenye no za madaktari wazuri hasa madaktari wa kike naomba waziweke no humu au kama hawana no basi wanipe japo jina la daktari na hosipitali anayo tibia.
 
Hospitali ya Taifa Muhimbili ni bora zaid hizi za Private ni Profit oriented wanalazimishaga operatin ili wapate pesa

Asante nduguyangu, ila nasikia Kuna kuwa na foleni sana. Ngoja najaribu kufuatilia.
 
Kwa mahudhurio makini ya clinic nenda Haemeda pale Upanga makao makuu ya scout wapo madaktari wazuri sana ila ikifika muda wa kujifungua aende Muhimbili fast track kuko poa sana.
 
Denguhiy15260233 said:
Kwa mahudhurio makini ya clinic nenda Haemeda pale Upanga makao makuu ya scout wapo madaktari wazuri sana ila ikifika muda wa kujifungua aende Muhimbili fast track kuko poa sana.
Asante Mkuu, hiyo Hemeda ndio naisikia ntafuatilia
 
Asante Mkuu, una weza kunipa uzoefu kidogo wa muhimbili kama gharama zao katika hicho kitengo cha private etc.
Kitengo cha private sijui, mi nilihudhuria pale clinic na nlijifungulia pale kwa Bima sikutoa hata senti, huduma zilikuwa nzuri
 
Back
Top Bottom