Hongereni sana Azam Media Ltd

Hongereni sana Azam Media Ltd

Betterhalf

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
2,882
Reaction score
2,561
Habari za leo wana JF.
Poleni kwa mihangaiko ya kutwa nzima.
Leo tunaelekea kuuaga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka 2018.
Pamoja na majukumu mengine, Azam Media wameandaa kitu muhimu,mahsusi na cha kipekee kwa Watanzania na watazamaji na wafuatiliaji wa vipindi vyao kote ulimwenguni(ambako matangazo yao yanafika).
Kupitia Azam Two, wameendesha program ya pekee tangu majira ya saa 2 asubuhi kupitia studio zao za muda pale Mlimani City.Hongereni sana kwa hili.
Kupitia chaneli hiyo, wamekuwa na mahojiano na makundi mbalimbali wakiwamo wanasiasa,wachumi,wasanii,watu maarufu ambao wamefanyiwa interview ya wazi kupitia timu ya watangazaji mahiri wa Azam Media chini ya Comrade Tido Mhando.
Ama kweli mko vizuri sana na hongereni kwa ubunifu ambao umeonesha namna mnavyojali wateja wenu.
Vipindi vya leo vimekuwa na mtazamo tofauti.Wapo walioona kuwa ni sehemu ya kuwapumzisha wateja wenu kwa kuwapa ladha tofauti kutoka yale waliyoyazoea siku zote.Wengine, wamechukulia tukio hili kama sehemu ya kufanya muhtasari wa yale yote yaliyojiri mwaka 2017 kupitia vipindi vyenu kwenye maeneo ya siasa,uchumi,michezo,starehe na burudani pamoja na nyanja nyingine za kijamii.
Nawashauri wengine muige yale yafanywayo na Azam Media kuanzia na hili.
Hongereni sana Azam Media na staff nzima ya Uhai Production.
Kongole kwenu...!
 
azam huwa nawakubali sana najua wao hawatishwi na kodi, hawa wengine wakigusiwa kodi tu haooo mbio
Sure...jamaa wamejipanga sana.Wamepangilia vitu vizuri.Kila kundi lililokuwa pale Mlimani City lilikuwa kivutio.
Kwa Mfano;
1.Dr Shoo,Nape na Mtatiro-Hali ya kisiasa.
2.Prof Lipumba,Dr.... na Mh.Bashe-Hali ya kiuchumi.
3.Dr Shika- mtu maarufu.
4.Comedians- Gala Comedy.
N.k.
 
Jamaa nawashukuru maana wameniletea ligi zangu pendwa gheto hapa VPL kule La Liga....kwa mfano leo nimeshuhudia timu yangu pendwa ikikandwa mbili bila nikiwa kwenye kochi...
 
Jamaa nawashukuru maana wameniletea ligi zangu pendwa gheto hapa VPL kule La Liga....kwa mfano leo nimeshuhudia timu yangu pendwa ikikandwa mbili bila nikiwa kwenye kochi...
Kama unateleza tu....Big Up Azam Media.
Now tuungisheni na EPL TV live commentary badala ya radio commentary ya MUTV.
 
Azam wako makini sana,wanastahili pongezi.
 
Back
Top Bottom